Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Wafilipi 4:14-23

Wafilipi 4:14-23 SRUV

Lakini mlifanya vema, mliposhiriki nami katika dhiki yangu. Nanyi pia, ninyi wenyewe mnajua, enyi Wafilipi, ya kuwa katika mwanzo wa Injili, nilipotoka Makedonia, hakuna kanisa lingine lililoshirikiana nami katika habari hii ya kutoa na kupokea, ila ninyi peke yenu. Kwa kuwa hata huko Thesalonike mliniletea msaada kwa mahitaji yangu, wala si mara moja. Si kwamba nakitamani kile kipawa, bali nayatamani mazao yanayozidi kuwa mengi, katika hesabu yenu. Lakini ninavyo vitu vyote na kuzidi, tena nimejaa tele; nimepokea kwa mkono wa Epafrodito vitu vile vilivyotoka kwenu, harufu ya manukato, sadaka yenye kibali, impendezayo Mungu. Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu. Sasa atukuzwe Mungu, Baba yetu, milele na milele. Amina. Mnisalimie kila mtakatifu katika Kristo Yesu. Ndugu walio pamoja nami wanawasalimu. Watakatifu wote wanawasalimu, hasa wao walio wa nyumbani mwa Kaisari. Neema ya Bwana Yesu Kristo na iwe pamoja na roho zenu.

Soma Wafilipi 4