Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Marko 5:21-24

Marko 5:21-24 SRUV

Hata Yesu alipokwisha kuvuka kurudia ng'ambo katika ile mashua, wakamkusanyikia mkutano mkuu; naye alikuwa kando ya bahari. Akaja mtu mmoja katika wakuu wa sinagogi, jina lake Yairo; hata alipomwona, akaanguka miguuni pake, akimsihi sana, akisema, Binti yangu mdogo yuko karibu kufa; nakuomba uje, uweke mkono wako juu yake, apate kupona, na kuishi. Akaenda pamoja naye; mkutano mkuu wakamfuata, wakimsongasonga.

Soma Marko 5

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Marko 5:21-24