Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mathayo 15:32-39

Mathayo 15:32-39 SRUV

Yesu akawaita wanafunzi wake, akasema, Nawahurumia mkutano, kwa kuwa yapata siku tatu wamekaa pamoja nami, wala hawana kitu cha kula, tena sitaki kuwaaga wakiwa na njaa, wasije wakazimia njiani. Wanafunzi wake wakamwambia, Tupate wapi mikate mingi hapa nyikani, hata kushibisha mkutano mkuu namna hii? Yesu akawaambia, Mnayo mikate mingapi? Wakasema, Saba, na visamaki vichache. Akawaagiza mkutano waketi chini; akaitwaa ile mikate saba na vile visamaki, akashukuru akavimega, akawapa wanafunzi wake, nao wanafunzi wakawapa makutano. Wakala wote wakashiba; wakayaokota mabaki ya vipande vya mikate makanda saba, yamejaa. Nao waliokula walikuwa wanaume elfu nne, bila kuhesabu wanawake na watoto. Akawaaga makutano, akapanda katika mashua, akaenda pande za Magadani.

Soma Mathayo 15

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Mathayo 15:32-39