Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Luka 6:46-49

Luka 6:46-49 SRUV

Na kwa nini mnaniita, Bwana, Bwana, lakini hamyatendi nisemayo? Kila mtu ajaye kwangu, na kuyasikia maneno yangu na kuyatenda, nitawaonesha mfano wake. Mfano wake ni mtu ajengaye nyumba, na kuchimba chini sana, na kuweka msingi juu ya mwamba; na kulipokuja gharika, mto uliipiga nyumba ile kwa nguvu, usiweze kuitikisa; kwa kuwa imejengwa vizuri. Lakini yule aliyesikia ila hakutenda, mfano wake ni mtu aliyejenga nyumba juu ya ardhi pasipokuwa na msingi, mto ukaipiga kwa nguvu, ikaanguka mara; na maangamizi yake nyumba ile yakawa makubwa.

Soma Luka 6