Ayubu 26:1-4
Ayubu 26:1-4 SRUV
Ndipo Ayubu akajibu, na kusema, Jinsi ulivyomsaidia huyo asiye na uwezo! Jinsi ulivyouokoa mkono usio na nguvu! Jinsi ulivyomshauri huyo asiye na hekima! Na kutangaza ujuzi wa kweli kwa wingi! Je! Umetamka maneno kwa nani? Kisha ni roho ya nani iliyotoka kwako?