Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ezekieli 29:17-21

Ezekieli 29:17-21 SRUV

Ikawa katika mwaka wa ishirini na saba, mwezi wa kwanza, siku ya kwanza ya mwezi, neno la BWANA likanijia, kusema, Mwanadamu, Nebukadneza, mfalme wa Babeli, alilifanyisha jeshi lake kazi ngumu juu ya Tiro; kila kichwa kilitiwa upara, na kila bega liliambuliwa ngozi, lakini hakuna mshahara uliotoka Tiro, sio wake wala wa jeshi lake, kwa kazi ile aliyofanya juu yake. Basi, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nitampa Nebukadneza, mfalme wa Babeli, hiyo nchi ya Misri; naye atawachukua watu wake jamii yote pia, na kutwaa mateka yake, na kutwaa mawindo yake, nayo yatakuwa ndio mshahara wa jeshi lake. Nimempa nchi ya Misri kuwa malipo ya kazi aliyofanya, kwa sababu walifanya kazi kwa ajili yangu; asema Bwana MUNGU. Siku ile nitawachipushia nyumba ya Israeli pembe, nami nitakujalia kufumbua kinywa kati yao; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Ezekieli 29:17-21

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha