Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kutoka 33:7-11

Kutoka 33:7-11 SRUV

Basi desturi ya Musa, ilikuwa kuitwaa ile hema, na kuikita nje ya kambi na mbali hiyo kambi; akaiita, hema ya kukutania. Hata kila mtu aliyekuwa akitaka neno kwa BWANA, akatoka, akaenda hata hema ya kukutania, iliyokuwa nje ya kambi. Hata Musa alipotoka kuiendea ile hema, watu wote waliondoka wakasimama, kila mtu mlangoni pa hema yake, akamtazama Musa, hata alipokwisha kuingia hemani. Ikawa Musa alipoingia humo hemani, ile nguzo ya wingu ikashuka, ikasimama mlangoni pa ile hema; naye BWANA akasema na Musa. Watu wote wakaiona nguzo ya wingu ikisimama penye mlango wa hema; watu wote wakaondoka wakasujudu, kila mtu mlangoni pa hema yake. Naye BWANA akasema na Musa uso kwa uso, kama vile mtu asemavyo na rafiki yake. Kisha akageuka akarejea hata kambini; bali mtumishi wake Yoshua, mwana wa Nuni, naye ni kijana, hakutoka mle hemani.

Soma Kutoka 33

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Kutoka 33:7-11