Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mhubiri 1

1
Ubatili wa maisha
1Maneno ya Mhubiri#1:1 Mhubiri: Kiebrania ni Kohelethi, yaani, Mhubiri au Mshauri. mwana wa Daudi, mfalme katika Yerusalemu 2#Zab 39:5; 62:9,10; Mhu 4:4-6; Rum 8:20 Mhubiri asema, Ubatili mtupu, ubatili mtupu, mambo yote ni ubatili. 3#Mhu 3:9 Mtu ana faida gani ya kazi yake yote aifanyayo chini ya jua?
4 # Zab 104:5; 2 Pet 3:10 Kizazi huenda, kizazi huja; nayo dunia hudumu daima. 5#Zab 19:5 Jua lachomoza, na jua lashuka, na kufanya haraka kwenda mahali pa maawio yake. 6#Yn 3:8 Upepo huvuma kuelekea kusini, kisha huvuma kuelekea kaskazini; hugeuka daima katika mwendo wake, nao huyarudia mazunguko yake. 7#Ayu 38:10; Zab 104:8 Mito yote huingia baharini, lakini bahari haijai; huko iendako mito, ndiko irudiko tena.
8 # Mhu 3:1; Mit 27:20 Mambo yote yamejaa uchovu usioneneka, jicho halishibi kuona, wala sikio halikinai kusikia.
9 # Mwa 8:22; Mhu 3:15 Yaliyokuwako ndiyo yatakayokuwako; na yaliyotendeka ndiyo yatakayotendeka; wala jambo jipya hakuna chini ya jua. 10Je! Kuna jambo lolote ambalo watu husema juu yake, Tazama, ni jambo jipya? Limekwisha kuwako, tangu zamani za kale zilizokuwa kabla yetu sisi.
11Hakuna kumbukumbu lolote la vizazi vilivyotangulia; wala hakutakuwa na kumbukumbu lolote la vizazi vitakavyokuja, miongoni mwao wale watakaofuata baadaye.
Ubatili wa kutafuta hekima
12Mimi, Mhubiri, nilikuwa Mfalme wa Israeli katika Yerusalemu. 13#Mwa 3:19; Mhu 3:10 Nikatia moyo wangu ili kuyatafuta yote yanayotendeka chini ya mbingu, na kuyavumbua kwa hekima; ni taabu kubwa ambayo Mungu amewapa wanadamu, ili kutaabika ndani yake. 14Nimeziona kazi zote zifanywazo chini ya jua; na, tazama, mambo yote ni ubatili na kufukuza upepo.#1:14 au kujilisha upepo.
15 # Mhu 7:13 Yaliyopotoka hayawezi kunyoshwa,
Wala yasiyokuwapo hayahesabiki.
16 # 1 Fal 4:29-31; 3:12; Mhu 2:9 Nikatafakari nikisema, Nimejipatia hekima nyingi kupita wote walionitangulia katika Yerusalemu; naam, moyo wangu umeona kwa wingi hekima na maarifa. 17#Mhu 2:3; 1 The 5:21 Nikatia moyo wangu ili kuijua hekima, na kujua wazimu na upumbavu; nikatambua ya kwamba hayo yote nayo ni kufukuza upepo. 18#Ayu 28:28; Mhu 7:16; 1 Kor 1:20 Yaani,
Katika wingi wa hekima mna wingi wa huzuni;
Naye aongezaye maarifa huongeza masikitiko.

Iliyochaguliwa sasa

Mhubiri 1: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia