Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Samweli 20:13-26

2 Samweli 20:13-26 SRUV

Na alipoondolewa katika njia kuu, watu wote wakapita, wakamwandama Yoabu ili kumfuatia Sheba, mwana wa Bikri. Naye akapita kati ya kabila zote za Israeli mpaka Abeli, na kwa Bethmaaka na Wabikri wote; nao wakakusanyika, wakaenda pia kumwandama. Na hao wakaja wakauzingira katika Abeli wa Bethmaaka, wakafanya kilima mbele ya mji, nacho kikasimama kuielekea ngome; na watu wote waliokuwa pamoja na Yoabu wakavunjavunja ukuta, wapate kuubomoa. Ndipo akalia mwanamke mmoja mwenye hekima toka mjini, Sikieni, sikieni; mwambieni na Yoabu, aje hapa karibu, niseme naye. Basi akamkaribia; na yule mwanamke akasema, Ndiwe Yoabu? Akajibu, Ndimi. Ndipo akamwambia Sikia maneno ya mjakazi wako. Akajibu, Mimi nasikia. Kisha akanena, akisema, Watu hunena zamani za kale, wakisema, Wasikose kuuliza huko Abeli; ndivyo walivyoleta suluhu. Mimi ni mmoja wa hao wenye amani, walio waaminifu katika Israeli; wewe unataka kuuharibu mji ulio kama mama wa Israeli; mbona unataka kuumeza urithi wa BWANA? Yoabu akajibu, akasema, Isiwe, isiwe kwangu, niumeze wala kuuharibu. Neno hili silo hivyo; lakini mtu mmoja wa milima ya Efraimu, jina lake, Sheba, mwana wa Bikri, ameinua mkono wake juu ya mfalme, naam, Daudi, basi mtoeni yeye tu, nami nitaondoka katika mji huu. Basi yule mwanamke akamwambia Yoabu, Tazama, kichwa chake utatupiwa juu ya ukuta. Ndipo yule mwanamke akawaendea watu wote katika hekima yake. Nao wakamkata kichwa Sheba, mwana wa Bikri, wakamtupia Yoabu huko nje. Ndipo akapiga tarumbeta, nao wakatawanyika kutoka mjini kila mtu hemani kwake. Naye Yoabu akarudi mpaka Yerusalemu kwa mfalme. Basi Yoabu alikuwa akiongoza jeshi lote la Israeli; na Benaya, mwana wa Yehoyada, alikuwa akiwaongoza Wakerethi, na Wapelethi; na Adoramu alikuwa akiwaongoza Shokoa; na Yehoshafati, mwana wa Ahiludi, alikuwa mwekaji kumbukumbu; na Shausha mwandishi; na Sadoki na Abiathari walikuwa makuhani. Tena na Ira, Myairi, alikuwa kuhani kwa Daudi.