Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Petro 3:9-12

1 Petro 3:9-12 SRUV

watu wasiolipa baya kwa baya, au laumu kwa laumu; bali wenye kubariki; kwa sababu hayo ndiyo mliyoitiwa ili mrithi baraka. Kwa maana, Atakaye kupenda maisha, Na kuona siku njema, Auzuie ulimi wake usinene mabaya, Na midomo yake isiseme uongo. Na aache mabaya, atende mema; Atafute amani, aifuate sana. Kwa kuwa macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, Na masikio yake husikiliza maombi yao; Bali uso wa Bwana uko juu ya watenda mabaya.

Soma 1 Petro 3

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na 1 Petro 3:9-12