Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Wakorintho 11:2-10

1 Wakorintho 11:2-10 SRUV

Basi nawasifu, kwa sababu mmenikumbuka katika mambo yote, nanyi mmeyashika yale mapokeo vile vile kama nilivyowatolea. Lakini nataka mjue ya kuwa kichwa cha kila mwanamume ni Kristo, na kichwa cha mwanamke ni mwanamume, na kichwa cha Kristo ni Mungu. Kila mwanamume, asalipo, au anapotoa unabii, naye amefunikwa kichwa, anaaibisha kichwa chake. Bali kila mwanamke asalipo, au anapotoa unabii, bila kufunika kichwa, anaaibisha kichwa chake; kwa maana ni sawasawa na yule aliyenyolewa. Maana mwanamke asipojifunika kichwa, na akatwe nywele. Au ikiwa ni aibu mwanamke kukatwa nywele zake au kunyolewa, na afunike kichwa. Kwa maana kweli haimpasi mwanamume kufunikwa kichwa, kwa sababu yeye ni mfano na utukufu wa Mungu. Lakini mwanamke ni utukufu wa mwanamume. Maana mwanamume hakutoka katika mwanamke, bali mwanamke katika mwanamume. Wala mwanamume hakuumbwa kwa ajili ya mwanamke, bali mwanamke kwa ajili ya mwanamume. Kwa hiyo imempasa mwanamke awe na dalili ya kumilikiwa kichwani, kwa ajili ya malaika.