Zab 85
85
Sala ya Kupata Fadhili za Mungu Tena
Kwa mwimbishaji. Ya Wakorahi. Zaburi.
1 #
Yer 30:18; Eze 39:25 BWANA, umeiridhia nchi yako,
Umewarejeza mateka wa Yakobo.
2Umeusamehe uovu wa watu wako,
Umezisitiri hatia zao zote.
3Umeiondoa ghadhabu yako yote,
Umerudi na kuuacha ukali wa hasira yako.
4Mungu wa wokovu wetu, uturudishe,
Uikomeshe hasira uliyo nayo juu yetu.
5Je! Utatufanyia hasira hata milele?
Utadumisha ghadhabu kizazi hata kizazi?
6 #
Hab 3:2
Je! Hutaki kurudi na kutuhuisha,
Watu wako wakufurahie?
7Ee BWANA, utuonyeshe rehema zako,
Utupe wokovu wako.
8 #
Hab 2:1; Zek 9:10; 2 Pet 2:20 Na nisikie atakavyosema Mungu BWANA,
Maana atawaambia watu wake amani,
Naam, na watauwa wake pia,
Bali wasiurudie upumbavu tena.
9Hakika wokovu wake u karibu na wamchao,
Utukufu ukae katika nchi yetu.
10 #
Mik 7:20; Yn 1:17; Zab 72:2,3; Isa 32:17; Lk 2:14; Yn 14:27 Fadhili na kweli zimekutana,
Haki na amani zimehusiana.
11 #
Isa 45:8; 2 Kor 5:14-21 Kweli imechipuka katika nchi,
Haki imechungulia kutoka mbinguni.
12 #
Yak 1:17
Naam, BWANA atatoa kilicho chema,
Na nchi yetu itatoa mazao yake.
13Haki itakwenda mbele zake,
Nayo itazifanya hatua zake kuwa njia.
Iliyochaguliwa sasa
Zab 85: SUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.