Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 73:21-28

Zab 73:21-28 SUV

Moyo wangu ulipoona uchungu, Viuno vyangu viliponichoma, Nalikuwa kama mjinga, sijui neno; Nalikuwa kama mnyama tu mbele zako. Walakini mimi ni pamoja nawe daima, Umenishika mkono wa kuume. Utaniongoza kwa shauri lako, Na baadaye utanikaribisha kwa utukufu. Ni nani niliye naye mbinguni, Wala duniani sina cha kupendeza ila Wewe. Mwili wangu na moyo wangu hupunguka, Bali Mungu ni mwamba wa moyo wangu Na sehemu yangu milele. Maana wajitengao nawe watapotea; Umewaangamiza wote waliokuacha Wewe. Nami kumkaribia Mungu ni kwema kwangu; Nimefanya kimbilio kwa Bwana MUNGU, Niyahubiri matendo yako yote.