Zab 64
64
Sala ya Ulinzi kutoka kwa Adui
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.
1Mungu, uisikie sauti yangu katika malalamiko yangu;
Unilinde uhai wangu na hofu ya adui.
2 #
Zab 143:9
Utanificha mbali na shauri la siri la watenda mabaya,
Mbali na ghasia ya watu wafanyao maovu;
3 #
Zab 57:4
Waliounoa ulimi wao kama upanga,
Wameielekeza mishale yao, maneno ya uchungu,
4Wapate kumpiga mkamilifu faraghani,
Kwa ghafula humpiga wala hawaogopi.
5Walijifanya hodari katika jambo baya;
Hushauriana juu ya kutega mitego;
Husema, Ni nani atakayeiona?
6Hutunga maovu; husema, Tumefanya shauri kamili;
Na mawazo ya ndani ya kila mmoja wao,
Na moyo wake, huwa siri kabisa.
7Kwa hiyo Mungu atawapiga shabaha,
Kwa mshale mara watapigwa.
8 #
Mit 12:13
Ndivyo watakavyokwazwa,
Ulimi wao wenyewe ukishindana nao.
Wote wawaonao watatikisa kichwa.
9Na watu wote wataogopa,
Wataitangaza kazi ya Mungu,
Na kuyafahamu matendo yake.
10 #
Zab 32:11; Flp 4:4 Mwenye haki atamfurahia BWANA na kumkimbilia,
Na wote wenye moyo wa adili watajisifu.
Iliyochaguliwa sasa
Zab 64: SUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.