Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 132

132
Maskani ya Milele ya Mungu katika Sayuni
Wimbo wa kupanda mlima.
1BWANA, umkumbukie Daudi
Taabu zake zote alizotaabika.
2Ndiye aliyemwapia BWANA,
Akaweka nadhiri kwa Shujaa wa Yakobo.
3Sitaingia hemani mwa nyumba yangu,
Wala sitapanda matandiko ya kitanda changu;
4 # Rut 3:18 Sitaacha macho yangu kuwa na usingizi,
Wala kope zangu kusinzia;
5Hata nitakapompatia BWANA mahali,
Na Shujaa wa Yakobo maskani.
6 # Yos 18:1; 1 Nya 13:5; 2 Nya 6:41-42; 1 Sam 17:12; 7:1 Tazama, tulisikia habari zake katika Efrata,
Katika konde la Yearimu tuliiona.
7Na tuingie katika maskani yake,
Tusujudu penye kiti cha kuwekea miguu yake.
8 # Hes 10:35 Ee BWANA, uinuke, uende kwenye raha yako,
Wewe na sanduku la nguvu zako.
9 # Ayu 29:14; Isa 61:10 Makuhani wako na wavikwe haki,
Watauwa wako na washangilie.
10Kwa ajili ya Daudi, mtumishi wako,
Usiurudishe nyuma uso wa masihi#132:10 Au, mtiwa mafuta. wako.
11 # 1 Fal 8:25; 2 Sam 7:12-16; 1 Nya 6:16; 1 Nya 17:11-14; Zab 89:4-5; Lk 1:69; Mdo 2:30 BWANA amemwapia Daudi neno la kweli,
Hatarudi nyuma akalihalifu,
Baadhi ya wazao wa mwili wako
Nitawaweka katika kiti chako cha enzi.
12Wanao wakiyashika maagano yangu,
Na shuhuda nitakazowafundisha;
Watoto wao nao wataketi
Katika kiti chako cha enzi milele.
13Kwa kuwa BWANA ameichagua Sayuni,
Ameitamani akae ndani yake.
14Hapo ndipo mahali pangu pa raha milele,
Hapo nitakaa kwa maana nimepatamani.
15Hakika nitavibariki vyakula vyake
Wahitaji wake nitawashibisha chakula.
16 # 2 Nya 6:41; Hos 11:12 Na makuhani wake nitawavika wokovu,
Na watauwa wake watashangilia.
17 # 1 Fal 11:36; Zab 92:10; Eze 29:21; Lk 1:69 Hapo nitamchipushia Daudi pembe,
Na taa nimemtengenezea masihi#132:17 Au, mtiwa mafuta. wangu.
18Adui zake nitawavika aibu,
Bali juu yake taji yake itasitawi.

Iliyochaguliwa sasa

Zab 132: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia