Mit 1:1-7
Mit 1:1-7 SUV
Mithali za Sulemani, mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli. Kujua hekima na adabu; kutambua maneno ya ufahamu; kufundishwa matendo ya busara, katika haki na hukumu na adili. Kuwapa wajinga werevu, na kijana maarifa na hadhari; mwenye hekima asikie na kuongezewa elimu, na mwenye ufahamu ayafikie mashauri yenye njia. Kufahamu mithali na kitendawili, na maneno ya wenye hekima na mafumbo yao. Kumcha BWANA ni chanzo cha maarifa, Bali wapumbavu hudharau hekima na adabu.