Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Hes 6

6
Wanadhiri
1 # Law 27:2; Amu 13:5; Mdo 21:23; Rum 1:1 Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia, 2#Law 10:9; Amu 13:4; Amo 2:12; Lk 1:15Nena na watu wa Israeli, uwaambie, Mtu mume au mtu mke atakapoweka nadhiri kubwa, nadhiri ya Mnadhiri, ili ajiweke wakfu kwa BWANA; 3#Lk 1:15atajitenga na divai na vileo; hatakunywa siki ya divai, wala siki ya kileo, wala asinywe maji yo yote ya zabibu, wala asile zabibu, mbichi wala zilizokauka. 4Siku zote za kujitenga kwake asile kitu cho chote kilichoandaliwa kwa mzabibu, tangu kokwa hata maganda. 5#Amu 13:5; 1 Sam 1:11; Omb 4:7Siku zote za nadhiri yake ya kujitenga, wembe usimfikilie kichwani mwake; hata hizo siku zitakapotimia, ambazo alijiweka wakfu kwa BWANA, atakuwa mtakatifu, ataziacha nywele za kichwani mwake zikue ziwe ndefu. 6#Law 19:28; 21:11; Yer 16:5,6; Eze 24:16-18; Mt 8:21Siku hizo zote ambazo alijiweka awe wa BWANA asikaribie maiti. 7#Hes 9:6Hatajitia unajisi kwa ajili ya baba yake, wala kwa ajili ya mamaye, wala kwa nduguye mume, wala kwa umbu lake, wakifa wao; kwa sababu ya huku kujiweka kwa Mungu ni juu ya kichwa chake. 8Siku zote za kujitenga kwake, yeye ni mtakatifu kwa BWANA 9#Mdo 18:18Na kama mtu ye yote akifa ghafla karibu naye, akajitia unajisi kichwa cha kutengwa kwake, ndipo atakinyoa kichwa siku hiyo ya kutakaswa kwake, atakinyoa siku ya saba. 10#Law 5:7; 14:22Tena siku ya nane ataleta hua wawili, au makinda mawili ya njiwa, aende nao kwa kuhani, hata mlangoni pa hema ya kukutania; 11naye kuhani atasongeza mmoja kuwa sadaka ya dhambi, na wa pili kuwa sadaka ya kuteketezwa, naye atafanya upatanisho kwa ajili yake, kwa sababu aliingia kosani kwa ajili ya mfu, naye atatakasa kichwa chake siku iyo hiyo. 12Kisha ataziweka kwa BWANA hizo siku za kujitenga kwake, naye ataleta mwana-kondoo mume wa mwaka wa kwanza, kuwa sadaka ya hatia; lakini hizo siku za kwanza hazitahesabiwa, kwa kuwa kule kujitenga kwake kulitiwa unajisi.
13 # Mdo 21:23-24 Na sheria ya Mnadhiri ni hii, zitakapotimia hizo siku za kujitenga kwake; ataletwa mlangoni pa hema ya kukutania; 14#Law 4:2; 3:6naye atasongeza sadaka yake kwa BWANA, mwana-kondoo mmoja mume wa mwaka wa kwanza mkamilifu, kuwa sadaka ya kuteketezwa, na mwana-kondoo mmoja mke wa mwaka wa kwanza mkamilifu, kuwa sadaka ya dhambi, na kondoo mume mmoja mkamilifu kwa sadaka ya amani, 15#Law 2:4; 8:2; 9:4; Yn 6:50-53; Kut 29:2; Hes 15:5,7; Isa 62:9; Yoe 1:9,13; 1 Kor 10:31; 11:26na kikapu cha mikate isiyotiwa chachu, mikate ya unga mwembamba iliyokandwa kwa mafuta, na mikate ya kaki isiyochachwa, iliyotiwa mafuta, pamoja na sadaka zake za unga, na sadaka zake za kinywaji. 16Na kuhani atavisongeza mbele za BWANA, naye atasongeza sadaka yake ya dhambi, na sadaka yake ya kuteketezwa; 17naye atamsongeza huyo kondoo mume kuwa dhabihu ya sadaka za amani kwa BWANA, pamoja na kikapu cha mikate isiyotiwa chachu; kisha kuhani atasongeza sadaka ya unga nayo, na sadaka yake ya kinywaji. 18#Mdo 21:24; Lk 17:10; Rum 6:6; Gal 5:24; Efe 4:23; Kol 3:9Naye Mnadhiri atakinyoa kichwa cha kujitenga kwake, mlangoni pa hema ya kukutania, kisha atatwaa hizo nywele za kichwa cha kujitenga kwake, na kuzitia katika moto ulio chini ya dhabihu ya sadaka za amani. 19#Law 8:31; Kut 29:23,24Kisha kuhani atautwaa mkono wa huyo kondoo mume uliotokoswa, na mkate mmoja usio chachu atautwaa kikapuni, na mkate mmoja wa kaki, naye ataitia mikononi mwa yule Mnadhiri, baada ya kunyoa kichwa cha kujitenga kwake; 20#Law 9:21; Mhu 9:7; Isa 35:10; Yn 17:4,5; Ufu 14:13naye kuhani atavitikisa viwe sadaka ya kutikiswa mbele za BWANA; kitu hicho ni kitakatifu kwa kuhani, pamoja na kidari cha kutikiswa, na paja la kuinuliwa; kisha baadaye Mnadhiri ana ruhusa kunywa divai. 21Sheria ya Mnadhiri awekaye nadhiri ni hiyo, tena ni sheria ya sadaka yake atakayomtolea BWANA kwa ajili ya kujitenga kwake, pamoja na vitu vile ambavyo aweza kuvipata zaidi; kama nadhiri yake awekayo ilivyo, ndivyo impasavyo kufanya kwa kuiandama sheria ya kujitenga kwake.
Baraka ya Kikuhani
22Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia, 23#1 Nya 23:13Nena na Haruni na wanawe, uwaambie, Hivi ndivyo mtakavyowabarikia wana wa Israeli; mtawaambia;
24 # Zab 134:3; 121:7; Yn 17:11; 1 Pet 1:5 BWANA akubarikie, na kukulinda;
25 # Zab 67:1; 80:3; Dan 9:17; Mwa 43:29; Yn 1:17; Rum 5:21 BWANA akuangazie nuru za uso wake, na kukufadhili;
26 # Zab 21:6; Mdo 2:28; Zab 85:10; Isa 26:3,12; Lk 2:14; Yn 20:21; Rum 15:13; 2 The 3:16 BWANA akuinulie uso wake, na kukupa amani.
27 # Kum 28:10; 2 Nya 7:14; Zab 115:12 Ndivyo watakavyoweka jina langu juu ya wana wa Israeli; nami nitawabarikia.

Iliyochaguliwa sasa

Hes 6: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha