Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Hes 1

1
Hesabu ya Kwanza ya Waisraeli
1 # Hes 26:1-51; Kut 19:1; Law 27:34; Hes 10:12; Kut 25:22; Law 1:1 BWANA akanena na Musa katika bara ya Sinai, hemani mwa kukutania, siku ya kwanza ya mwezi wa pili, katika mwaka wa pili baada ya kutoka kwao nchi ya Misri, akamwambia, 2#Kut 30:12; 38:26; Hes 26:2-4,63,64; 1 Nya 21:2; 2 Sam 24:2Fanyeni hesabu ya mkutano wote wa wana wa Israeli, kwa kuandama jamaa zao, na nyumba za baba zao, kama hesabu ya majina ilivyo, kila mtu mume kichwa kwa kichwa; 3tangu mwenye miaka ishirini umri wake, na zaidi, wote wawezao kutoka kwenenda vitani katika Israeli; wewe na Haruni mtawahesabu kwa kuandama majeshi yao. 4#Hes 2:2; 1 Nya 27:1Tena mtu mume mmoja wa kila kabila atakuwa pamoja nanyi; kila mmoja aliye kichwa cha nyumba ya baba zake. 5#Mwa 29:32; Kut 1:2; Kum 33:6; Ufu 7:4Na majina ya hao waume watakaosimama pamoja nanyi ni haya; Wa Reubeni; Elisuri mwana wa Shedeuri. 6Wa Simeoni; Shelumieli mwana wa Suri-shadai. 7#Hes 7:12; 10:14; Rut 4:20; 1 Nya 2:10; Lk 3:32Wa Yuda; Nashoni mwana wa Aminadabu. 8Wa Isakari; Nethaneli mwana wa Suari. 9Wa Zabuloni; Eliabu mwana wa Heloni. 10Katika wana wa Yusufu; wa Efraimu, Elishama mwana wa Amihudi; na wa Manase; Gamalieli mwana wa Pedasuri. 11Wa Benyamini Abidani mwana wa Gideoni. 12Wa Dani; Ahiezeri mwana wa Amishadai. 13Wa Asheri; Pagieli mwana wa Okirani. 14#Hes 2:14Wa Gadi; Eliasafu mwana wa Deueli. 15Wa Naftali; Ahira mwana wa Enani. 16#Mwa 6:4; Kut 18:21; Hes 7:2; 1 Nya 5:24; Amu 6:15; Kut 18:21; Kum 1:15Hao ndio walioitwa wa mkutano, wakuu wa kabila za baba zao; nao ndio vichwa vya wale maelfu ya Israeli. 17Basi Musa na Haruni wakawatwaa hao watu waume waliotajwa majina yao; 18#Ezr 2:59; Neh 7:61; Ebr 7:3nao waliukutanisha mkutano mzima, siku ya kwanza ya mwezi wa pili, nao wakaonyesha ukoo wa vizazi vyao kwa kuandama jamaa zao, kwa nyumba za baba zao, kama hesabu ya majina, tangu umri wa miaka ishirini na zaidi, kichwa kwa kichwa. 19#Hes 26:1,2; 1 Nya 27:23,24; 2 Sam 24:1Kama BWANA alivyomwagiza Musa, ndivyo alivyowahesabu huko katika bara ya Sinai.
20Na wana wa Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Israeli, vizazi vyao, kwa kuandama jamaa zao, na nyumba za baba zao, kama hesabu ya majina, kichwa kwa kichwa, kila mtu mume tangu umri wa miaka ishirini na zaidi wote walioweza kwenda vitani; 21wale waliohesabiwa katika kabila ya Reubeni, walikuwa watu arobaini na sita elfu na mia tano (46,500).
22 # 2 Sam 22:35; Zab 44:3; 60:12; 1 Kor 16:13; 2 Kor 3:5; Efe 6:12 Katika wana wa Simeoni, vizazi vyao, kwa kuandama jamaa zao, na nyumba za baba zao, wale waliohesabiwa kama hesabu ya majina, kichwa kwa kichwa, kila mume tangu umri wa miaka ishirini na zaidi, wote walioweza kwenda vitani; 23wale waliohesabiwa katika kabila ya Simeoni, walikuwa watu hamsini na kenda elfu na mia tatu (59,300).
24 # Mwa 30:11; 49:19; Yos 4:12; Ufu 7:5 Katika wana wa Gadi, kwa kuandama vizazi vyao, jamaa zao, na nyumba za baba zao, kama hesabu ya majina, tangu umri wa miaka ishirini na zaidi, wote walioweza kwenda vitani; 25wale waliohesabiwa katika kabila ya Gadi, walikuwa watu arobaini na tano elfu na mia sita na hamsini (45,650).
26 # Mwa 29:35; 49:8-10; Zab 78:68; Mt 1:2; Ebr 7:14; Ufu 5:5 Katika wana wa Yuda, vizazi vyao, kwa kuandama jamaa zao, na nyumba za baba zao, kama hesabu ya majina, tangu umri wa miaka ishirini na zaidi, wote walioweza kwenda vitani; 27wale waliohesabiwa katika kabila ya Yuda, walikuwa watu sabini na nne elfu na mia sita (74,600).
28Katika wana wa Isakari, vizazi vyao, kwa kuandama jamaa zao, na nyumba za baba zao, kwa hesabu ya majina, tangu umri wa miaka ishirini na zaidi, wote walioweza kwenda vitani; 29wale waliohesabiwa katika kabila ya Isakari, walikuwa watu hamsini na nne elfu na mia nne (54,400).
30Katika wana wa Zabuloni, vizazi vyao, kwa kuandama jamaa zao, na nyumba za baba zao, kama hesabu ya majina, tangu umri wa miaka ishirini na zaidi, wote walioweza kwenda vitani; 31wale waliohesabiwa katika kabila ya Zabuloni, walikuwa watu hamsini na saba elfu na mia nne (57,400).
32 # Mwa 30:24; 48:15,20; Zab 60:7; 78:67; Yer 7:15 Katika wana wa Yusufu, maana katika wana wa Efraimu, vizazi vyao kwa kuandama jamaa zao, na nyumba za baba zao, kama hesabu ya majina, tangu umri wa miaka ishirini na zaidi, wote walioweza kwenda vitani, 33wale waliohesabiwa katika kabila ya Efraimu, walikuwa watu arobaini elfu na mia tano (40,500).
34Katika wana wa Manase, vizazi vyao, kwa kuandama jamaa zao, na nyumba za baba zao, kama hesabu ya majina, tangu umri wa miaka ishirini na zaidi, wote walioweza kwenda vitani; 35wale waliohesabiwa katika kabila ya Manase, walikuwa watu thelathini na mbili elfu na mia mbili (32,200). 36#Mwa 35:16-18; 44:20; 49:27; Zab 68:27; Ufu 7:8Katika wana wa Benyamini, vizazi vyao, kwa kuandama jamaa zao, na nyumba za baba zao, kama hesabu ya majina, tangu umri wa miaka ishirini na zaidi, wote walioweza kwenda vitani; 37wale waliohesabiwa katika kabila ya Benyamini, walikuwa watu thelathini na tano elfu na mia nne (35,400).
38 # Mwa 30:5,6; 49:16,17 Katika wana wa Dani, vizazi vyao, kwa kuandama jamaa zao, na nyumba za baba zao, kama hesabu ya majina, tangu umri wa miaka ishirini na zaidi, wote walioweza kwenda vitani; 39wale waliohesabiwa katika kabila ya Dani, walikuwa watu sitini na mbili elfu na mia saba (62,700).
40Katika wana wa Asheri, vizazi vyao, kwa kuandama jamaa zao, na nyumba za baba zao, kama hesabu ya majina, tangu umri wa miaka ishirini na zaidi, wote walioweza kwenda vitani; 41wale waliohesabiwa katika kabila ya Asheri, walikuwa watu arobaini na moja elfu na mia tano (41,500).
42Katika wana wa Naftali, vizazi vyao, kwa kuandama jamaa zao, na nyumba za baba zao, kama hesabu ya majina, tangu umri wa miaka ishirini na zaidi, wote walioweza kwenda vitani; 43wale waliohesabiwa katika kabila ya Naftali, walikuwa watu hamsini na tatu elfu na mia nne (53,400).
44 # Hes 26:64 Hao ndio waliohesabiwa, ambao Musa na Haruni na wale wakuu wa Israeli watu kumi na wawili waliwahesabu; walikuwa kila mmoja kwa ajili ya nyumba ya baba zake. 45Basi hao wote waliohesabiwa katika wana wa israeli kwa kuandama nyumba za baba zao tangu umri wa miaka ishirini na zaidi; wote walioweza kwenda vitani katika Israeli; 46#Mwa 13:16; Kut 12:37; 38:26; Kum 10:22; Hes 26:51; 1 Fal 4:20hao wote waliohesabiwa walikuwa ni watu waume mia sita na tatu elfu na mia tano na hamsini (603,550).
47 # Hes 2:33; 3:1; 26:57; 1 Nya 6:1; 21:6 Lakini Walawi kwa kuiandama kabila ya baba zao hawakuhesabiwa katika watu hao. 48Kwa kuwa BWANA alinena na Musa, na kumwambia, 49#Hes 26:62Hiyo kabila ya Lawi tu usiihesabu, wala usiitie hesabu yao katika wana wa Israeli; 50#Kut 31:18; 32:26; Hes 3:7,8,23; 4:15-33lakini uwaweke Walawi wawe juu ya maskani ya ushahidi, na juu ya vyombo vyake vyote, na juu ya vitu vyake vyote; wao wataichukua hiyo maskani, na vyombo vyake vyote; nao wataitumikia, na kupanga hema zao kwa kuizunguka maskani pande zote. 51#Hes 10:17,21Tena hapo maskani itakapokwenda mbele, Walawi wataishusha; tena hapo maskani itakaposimamishwa, Walawi wataisimamisha; na mgeni atakayekaribia atauawa. 52Na wana wa Israeli watazipanga hema zao, kila mtu katika marago yake mwenyewe, kila mtu hapo ilipo beramu yake mwenyewe, kama majeshi yao yalivyo. 53#Law 10:6; Hes 8:19; 16:46; 1 Sam 6:19; Hes 8:24; 1 Nya 23:32; 2 Nya 13:10Lakini Walawi watapanga hema zao kuizunguka maskani ya ushahidi pande zote, ili zisiwe hasira juu ya mkutano wa wana wa Israeli; kisha Walawi wataulinda ulinzi wa hiyo maskani ya ushahidi. 54Ndivyo walivyofanya wana wa Israeli; kama yote BWANA aliyomwagiza Musa, ndivyo walivyofanya.

Iliyochaguliwa sasa

Hes 1: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia