Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Neh 12

12
Orodha ya Makuhani na Walawi
1 # Ezr 2:1; Neh 10:2-8 Basi, hawa ndio makuhani na Walawi waliopanda na Zerubabeli, mwana wa Shealueli, na Yoshua; Seraya, Yeremia, Ezra; 2Amaria, Maluki, Hatushi; 3Shekania, Harimu, Meremothi; 4#Lk 1:5Ido, Ginethoni, Abia; 5Miyamini, Maazia, Bilgai; 6Shemaya, Yoyaribu, Yedaya; 7#Hag 1:1; Zek 3:1Salu, Amoki, Hilkia, Yedaya. Hawa walikuwa wakuu wa makuhani na ndugu zao siku za Yoshua.
8 # 1 Nya 16:8,41; Neh 11:17 Tena Walawi; Yeshua, Binui, Kadmieli, Sherebia, Yuda, na Matania, aliyekuwa juu ya shukrani, yeye na ndugu zake. 9Tena Bakbukia na Uno, ndugu zao, kuwaelekea kwa zamu.
10Naye Yoshua akamzaa Yoyakimu, Yoyakimu akamzaa Eliashibu, Eliashibu akamzaa Yoyada, 11Yoyada akamzaa Yohana, Yohana akamzaa Yadua.
12Na siku za Yoyakimu wakawako makuhani, wakuu wa mbari za mababa; wa Seraya, Meraya; wa Yeremia, Hanania; 13wa Ezra, Meshulamu; wa Amaria, Yehohanani; 14wa Maluki, Yonathani; wa Shekania, Yusufu; 15wa Harimu, Adna; wa Meremothi, Helkai; 16wa Ido, Zekaria; wa Ginethoni, Meshulamu; 17wa Abia, Zikri; wa Miyamini; wa Maazia, Piltai; 18wa Bilgai, Shamua; wa Shemaya, Yehonathani; 19wa Yoyaribu, Matenai; wa Yedaya, Uzi; 20wa Salu, Kalai; wa Amoki, Eberi; 21wa Hilkia, Hashabia; wa Yedaya, Nethaneli.
22Walawi siku za Eliashibu, na Yoyada, na Yohana, na Yadua, wameandikwa wakuu wa mbari za mababa; tena na makuhani; hata siku za kumiliki kwake Dario, Mwajemi. 23#1 Nya 9:14Wana wa Lawi, wakuu wa mbari za mababa, wameandikwa katika kitabu cha tarehe, hata siku za Yohana mwana wa Eliashibu. 24#1 Nya 23:1; 25:1; Ezr 3:11Nao wakuu wa Walawi; Hashabia, Sherebia, Yeshua, Binui, Kadmieli, na ndugu zao kuwaelekea, ili kusifu na kushukuru, kama amri ya Daudi, mtu wa Mungu, zamu kwa zamu. 25Matania, Bakbukia, Obadia, Meshulamu, Talmoni, na Akubu, walikuwa mabawabu, wa kulinda nyumba za hazina penye malango. 26#Neh 8:9; Ezr 7:6,11Hao walikuwapo siku za Yoyakimu, mwana ya Yoshua, mwana wa Yosadaki, na siku za Nehemia, liwali, na Ezra, kuhani, mwandishi.
Kuzinduliwa kwa Ukuta wa Mji
27 # Kum 20:5; 1 Nya 25:6; 2 Nya 5:13; Zab 81:1-3; Ufu 5:8 Basi, walipouweka wakfu ukuta wa Yerusalemu wakawatafuta Walawi katika mahali pao pote, ili kuwaleta Yerusalemu, wapate kufanya wakfu pamoja na furaha, na kwa shukrani, na kwa kuimba, kwa matoazi, vinanda na vinubi. 28Waimbaji wakakusanyika kutoka uwanda na viunga vya Yerusalemu, na kutoka vijiji vya Wanetofathi; 29tena toka Beth-gilgali, na toka mashamba ya Geba na Azmawethi; kwa maana waimbaji hao walikuwa wamejijengea vijiji katika viunga vya Yerusalemu. 30#Kut 19:10Makuhani na Walawi wakajitakasa, nao wakawatakasa watu, na malango, na ukuta. 31#Neh 2:13Ndipo nikawapandisha wakuu wa Yuda juu ya ukuta, nikawaagiza mikutano mikubwa miwili ya hao walioshukuru, na kuandamana; mmoja uende kwa kuume ukutani kuliendea lango la jaa; 32na baada yao wakaenda Hoshaya, na nusu ya wakuu wa Yuda, 33na Azaria, na Ezra, na Meshulamu, 34na Yuda, na Benyamini, na Shemaya, na Yeremia, 35#Hes 10:2; Yos 6:4; 2 Nya 5:12na baadhi ya makuhani wenye baragumu; Zekaria, mwana wa Yonathani, mwana wa Shemaya, mwana wa Matania, mwana wa Mikaya, mwana wa Zakuri, mwana wa Asafu; 36#1 Nya 23:5; 2 Nya 8:14; Amo 6:5na ndugu zake, Shemaya, Azareli, Milalai, Gilalai, Maai, Nethaneli, Yuda, na Hanani, wenye vinanda vya Daudi mtu wa Mungu; Ezra, mwandishi, akawatangulia; 37#Neh 2:14; 2 Sam 5:7-9; Neh 3:15,26na kwa lango la chemchemi, wakienda moja kwa moja mbele yao, wakapanda madaraja ya mji wa Daudi, uinukapo ukuta, juu ya nyumba ya Daudi, mpaka lango la maji upande wa mashariki. 38#Neh 3:8,11Na mkutano wa pili wao wenye kushukuru wakaenda kuwalaki, na mimi nikafuata nyuma yao, pamoja na nusu ya watu, ukutani juu ya mnara wa tanuu, mpaka ule ukuta mpana; 39#2 Fal 14:13; Neh 3:6; Yer 32:2na juu ya lango la Efraimu, na kupita lango la kale, na lango la samaki, na mnara wa Hananeli, na mnara wa Hamea, mpaka lango la kondoo; nao wakasimama hapo langoni pa gereza. 40#Zab 42:4Ndivyo walivyosimama mikutano miwili yao walioshukuru nyumbani mwa Mungu, na mimi, na nusu ya mashehe pamoja nami; 41na makuhani, Eliakimu, Maaseya, Miyamini, Mikaya, Elioenai, Zekaria na Hanania, wenye baragumu; 42na Maaseya, na Shemaya, na Eleazari, na Uzi, na Yehohanani, na Malkiya, na Elamu, na Ezeri. Waimbaji wakaimba kwa sauti kuu, wenye Yezrahia kuwa msimamizi wao. 43#Zab 9:2; 92:4Wakatoa dhabihu nyingi siku ile, wakafurahi; kwa kuwa Mungu amewafurahisha furaha kuu; na wanawake pia na watoto wakafurahi; hata ikasikiwa mbali sana furaha hiyo ya Yerusalemu.
Majukumu ya Hekaluni
44 # 2 Nya 13:11,12; Neh 13:5 Na siku hiyo watu wakaagizwa juu ya vyumba vya hazina, kwa sadaka za kuinuliwa, na kwa malimbuko, na kwa zaka, ili kuzikusanya, kwa kadiri ya mashamba ya miji, sehemu zilizoamriwa katika torati za makuhani, na Walawi; kwa maana Yuda waliwafurahia makuhani na Walawi waliotumika. 45#1 Nya 25:1Wakauangalia ulinzi wa Mungu wao, na ulinzi wa kutakasika, na hao waimbaji na mabawabu vile vile, sawasawa na amri ya Daudi, na ya Sulemani mwanawe. 46Kwa kuwa siku za Daudi zamani, Asafu alikuwa mkuu wa waimbaji, na juu ya nyimbo za sifa na shukrani kwa Mungu. 47Na Israeli wote, siku za Zerubabeli, na siku za Nehemia, walitoa sehemu za waimbaji na mabawabu, kama ilivyohusika kila siku; nao wakawatakasia Walawi; na Walawi wakawatakasia wana wa Haruni.

Iliyochaguliwa sasa

Neh 12: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha