Mk 8
8
Kuwalisha Watu Elfu Nne
1 #
Mt 15:32-39
Katika siku zile, kwa vile ulivyokuwa mkuu tena ule mkutano, nao wamekosa kitu cha kula, akawaita wanafunzi wake, akawaambia, 2#Mk 6:34-44Nawahurumia mkutano kwa sababu yapata siku tatu wamekaa nami, wala hawana kitu cha kula; 3nami nikiwaaga waende zao nyumbani kwao hali wanafunga, watazimia njiani; na baadhi yao wametoka mbali. 4Wanafunzi wake wakamjibu, Je! Ataweza wapi mtu kuwashibisha hawa mikate hapa nyikani? 5Akawauliza, Mnayo mikate mingapi? Wakasema, Saba, 6Akawaagiza mkutano waketi chini; akaitwaa ile mikate saba, akashukuru, akaimega, akawapa wanafunzi wake wawaandikie; wakawaandikia mkutano. 7Walikuwa na visamaki vichache; akavibarikia, akasema wawaandikie na hivyo pia. 8#Kum 28:5Wakala, wakashiba, wakakusanya mabaki ya vipande vya mikate makanda saba. 9Na watu waliokula wapata elfu nne. Akawaaga. 10Mara akapanda chomboni pamoja na wanafunzi wake, akaenda pande za Dalmanutha.
Dai la Ishara
11 #
Mt 16:1-12
#
Mt 12:38; Lk 11:16; Yn 6:30 Wakatokea Mafarisayo, wakaanza kuhojiana naye; wakitafuta kwake ishara itokayo mbinguni; wakimjaribu. 12#Mt 12:39; Lk 11:29Akaugua rohoni mwake, akasema, Mbona kizazi hiki chatafuta ishara? Amin, nawaambieni, Hakitapewa ishara kizazi hiki. 13Akawaacha, akapanda tena chomboni, akaenda zake hata ng’ambo.
Chachu ya Mafarisayo na ya Herode
14Wakasahau kuchukua mikate, wala chomboni hawana ila mkate mmoja tu. 15#Lk 12:1; Mk 3:6Akawaagiza, akasema, Angalieni, jihadharini na chachu ya Mafarisayo na chachu ya Herode. 16Wakabishana wao kwa wao, kwa kuwa hawana mikate. 17#Mk 6:52Naye Yesu akatambua, akawaambia, Mbona mnabishana kwa sababu hamna mikate? Hamfahamu bado, wala hamjaelewa? Je! Mioyo yenu ni mizito? 18#Yer 5:21; Eze 12:2; Mk 4:12Mna macho, hamwoni; mna masikio, hamsikii? Wala hamkumbuki? 19#Mk 6:41-44Nilipoivunja ile mikate mitano na kuwapa wale elfu tano, mlichukua vikapu vingapi vimejaa vipande? Wakamwambia, Kumi na viwili. 20#Mk 8:6-9Na ile saba kuwapa wale elfu nne, mlichukua makanda mangapi yamejaa vipande? Wakamwambia, Saba. 21Akawaambia, Hamjafahamu bado?
Yesu Amponya Kipofu Bethsaida
22 #
Mk 6:56
Wakafika Bethsaida, wakamletea kipofu, wakamsihi amguse. 23#Mk 7:32,33; Yn 9:6Akamshika mkono yule kipofu, akamchukua nje ya kijiji, akamtemea mate ya macho, akamwekea mikono yake, akamwuliza, Waona kitu? 24Akatazama juu, akasema, Naona watu kama miti, inakwenda. 25Ndipo akaweka tena mikono yake juu ya macho yake, naye akatazama sana; akawa mzima, akaona vyote waziwazi. 26#Mk 7:36Akampeleka nyumbani kwake, akisema, Hata kijijini usiingie.
27 #
Mt 16:13-28; Lk 9:18-27 Akatoka Yesu na wanafunzi wake, wakaenda kwenye vijiji vya Kaisaria-Filipi; na njiani akawauliza wanafunzi wake, akasema, Watu huninena mimi kuwa ni nani? 28#Mk 6:14-15; Lk 9:7-8Wakamjibu, Yohana Mbatizaji; wengine, Eliya; wengine, Mmojawapo wa manabii. 29#Yn 6:68-69Naye akawauliza, Na ninyi mnasema ya kuwa mimi ni nani? Petro akamjibu, akamwambia, Wewe ndiwe Kristo. 30#Mk 9:9Akawaonya wasimwambie mtu habari zake.
Yesu Asema juu ya Kufa na Kufufuka kwake
31Akaanza kuwafundisha kwamba imempasa Mwana wa Adamu kupatikana na mateso mengi, na kukataliwa na wazee, na wakuu wa makuhani, na waandishi, na kuuawa, na baada ya siku tatu kufufuka. 32Naye alikuwa akinena neno hilo waziwazi. Petro akamchukua, akaanza kumkemea. 33Akageuka, akawatazama wanafunzi wake, akamkemea Petro, akasema, Nenda nyuma yangu, Shetani; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu. 34#Mt 10:38; Lk 14:27Akawaita mkutano pamoja na wanafunzi wake, akawaambia, Mtu ye yote akitaka kunifuata na ajikane mwenyewe, ajitwike na msalaba wake, anifuate. 35#Mt 10:39; Lk 17:33; Yn 12:25Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake, ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya Injili, huyu ataisalimisha. 36Kwa kuwa itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote, akipata hasara ya nafsi yake? 37Ama mtu atoe nini badala ya nafsi yake? 38#Mt 10:33Maana kila mtu atakayenionea haya mimi, na maneno yangu, katika kizazi hiki cha uzinzi na dhambi, Mwana wa Adamu atamwonea haya mtu huyo, atakapokuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika watakatifu.
Iliyochaguliwa sasa
Mk 8: SUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.