YouVersion Logo
Search Icon

Mk 4:35, 36, 37, 38, 39, 40

Mk 4:35 SUV

Siku ile kulipokuwa jioni, akawaambia, Na tuvuke mpaka ng’ambo.

Mk 4:36 SUV

Wakauacha mkutano, wakamchukua vile vile alivyo katika chombo. Na vyombo vingine vilikuwako pamoja naye.

Mk 4:37 SUV

Ikatokea dhoruba kuu ya upepo, mawimbi yakakipiga chombo hata kikaanza kujaa maji.

Mk 4:38 SUV

Naye mwenyewe alikuwapo katika shetri, amelala juu ya mto; wakamwamsha, wakamwambia, Mwalimu, si kitu kwako kuwa tunaangamia?

Mk 4:39 SUV

Akaamka, akaukemea upepo, akaiambia bahari, Nyamaza, utulie. Upepo ukakoma, kukawa shwari kuu.

Mk 4:40 SUV

Akawaambia, Mbona mmekuwa waoga? Hamna imani bado?

Video for Mk 4:35-40