YouVersion Logo
Search Icon

Mk 14:1, 2, 3, 4, 5, 6, 7, 8, 9, 10, 11

Mk 14:1 SUV

Baada ya siku mbili ilikuwa sikukuu ya Pasaka, na mikate isiyochachwa; wakuu wa makuhani na waandishi wakatafuta njia ya kumkamata kwa hila na kumwua.

Mk 14:2 SUV

Kwa maana walisema, Isiwe kwa wakati wa sikukuu, isije ikatokea ghasia katika watu.

Mk 14:3 SUV

Naye alipokuwapo Bethania, nyumbani mwa Simoni mkoma, ameketi chakulani, alikuja mwanamke mwenye kibweta cha marhamu ya nardo safi ya thamani nyingi; akakivunja kibweta akaimimina kichwani pake.

Mk 14:4 SUV

Palikuwa na watu waliochukizwa katika nafsi zao wakisema, Kwani kupoteza marhamu namna hii?

Mk 14:5 SUV

Maana marhamu hii ingaliweza kuuzwa kwa dinari mia tatu na kuzidi, wakapewa maskini. Wakamnung’unikia sana yule mwanamke.

Mk 14:6 SUV

Yesu akasema, Mwacheni; mbona mnamtaabisha? Amenitendea kazi njema

Mk 14:7 SUV

maana sikuzote mnao maskini pamoja nanyi, na kila mpendapo mwaweza kuwatendea mema; lakini mimi hamnami sikuzote.

Mk 14:8 SUV

Ametenda alivyoweza; ametangulia kuupaka mwili wangu marhamu kwa ajili ya maziko.

Mk 14:9 SUV

Amin, nawaambia, Kila ihubiriwapo Injili katika ulimwengu wote, na hili alilotenda huyu litatajwa kwa kumbukumbu lake.

Mk 14:10 SUV

Yuda Iskariote, yule mmoja katika wale Thenashara, akaenda zake kwa wakuu wa makuhani, apate kumsaliti kwao.

Mk 14:11 SUV

Nao waliposikia walifurahi, wakaahidi kumpa fedha. Akatafuta njia ya kumsaliti wakati wa kufaa.