YouVersion Logo
Search Icon

Mk 13:1, 2, 3, 4, 5, 6, 7, 8, 9, 10, 11, 12, 14, 15, 16, 17, 18, 19, 20, 21, 22, 23, 24, 25, 26, 27, 28, 29, 30, 31

Mk 13:1 SUV

Hata alipokuwa akitoka hekaluni, mmoja wa wanafunzi wake alimwambia, Mwalimu, tazama, yalivyo mawe na majengo haya!

Mk 13:2 SUV

Yesu akajibu, akamwambia, Wayaona majengo haya makubwa? Halitasalia hapa jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomolewa.

Mk 13:3 SUV

Hata alipokuwa ameketi katika mlima wa Mizeituni, kuelekea hekalu Petro, na Yakobo, na Yohana, na Andrea walimwuliza kwa faragha

Mk 13:4 SUV

Tuambie, mambo hayo yatakuwa lini? Nayo ni nini dalili ya wakati, hayo yote yatakapokuwa karibu kutimia?

Mk 13:5 SUV

Yesu akaanza kuwaambia, Jihadharini, mtu asiwadanganye.

Mk 13:6 SUV

Wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi ndiye, nao watadanganya wengi.

Mk 13:7 SUV

Nanyi mtakaposikia habari za vita na uvumi wa vita, msitishwe; hayo hayana budi kutukia, lakini ule mwisho bado.

Mk 13:8 SUV

Kwa maana taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme; kutakuwa na matetemeko ya nchi mahali mahali; kutakuwako na njaa; hayo ndiyo mwanzo wa utungu.

Mk 13:9 SUV

Nanyi jihadharini nafsi zenu; maana watawapeleka ninyi mabarazani; na katika masinagogi mtapigwa; nanyi mtachukuliwa mbele ya maliwali na wafalme kwa ajili yangu, kuwa ushuhuda kwao.

Mk 13:10 SUV

Na sharti Injili ihubiriwe kwanza katika mataifa yote.

Mk 13:11 SUV

Na watakapowachukua ninyi, na kuwasaliti, msitafakari kwanza mtakayosema, lakini lo lote mtakalopewa saa ile, lisemeni; kwa maana si ninyi msemao, bali ni Roho Mtakatifu.

Mk 13:12 SUV

Na ndugu atamsaliti ndugu yake ili auawe, na baba atamsaliti mtoto, na watoto watashambulia wazazi wao, na kuwafisha.

Mk 13:14 SUV

Lakini mlionapo chukizo la uharibifu likisimama pasipolipasa, (asomaye na afahamu), ndipo walio katika Uyahudi na wakimbilie milimani

Mk 13:15 SUV

na mtu aliye juu ya dari asishuke, wala asiingie kuchukua kitu nyumbani mwake

Mk 13:16 SUV

naye aliye shambani asirudi nyuma kulichukua vazi lake.

Mk 13:17 SUV

Lakini ole wao wenye mimba, nao wanyonyeshao siku hizo!

Mk 13:18 SUV

Ila ombeni yasitokee hayo wakati wa baridi.

Mk 13:19 SUV

Kwa maana siku hizo zitakuwa na dhiki, jinsi isivyokuwa tangu mwanzo wa kuumba alipoumba Mungu hata sasa, wala haitakuwa kamwe.

Mk 13:20 SUV

Na kama Bwana asingalizikatiza siku hizo, asingeokoka mtu ye yote; lakini kwa ajili ya wateule aliowateua amezikatiza siku hizo.

Mk 13:21 SUV

Na wakati huo mtu akiwaambia, Tazama, Kristo yupo hapa, au yuko kule, msisadiki

Mk 13:22 SUV

kwa maana wataondoka Makristo wa uongo, na manabii wa uongo, watatoa ishara na maajabu, wapate kuwadanganya, kama yamkini, hata hao wateule.

Mk 13:23 SUV

Bali ninyi jihadharini; nimekwisha kuwaonya yote mbele.

Mk 13:24 SUV

Lakini siku zile, baada ya dhiki hiyo, jua litatiwa giza, na mwezi hatautoa mwanga wake.

Mk 13:25 SUV

na nyota za mbinguni zitakuwa zikianguka, na nguvu zilizo mbinguni zitatikisika.

Mk 13:26 SUV

Hapo ndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija mawinguni kwa nguvu nyingi na utukufu.

Mk 13:27 SUV

Ndipo atakapowatuma malaika na kuwakusanya wateule wake toka pepo nne, toka upande wa mwisho wa nchi hata upande wa mwisho wa mbingu.

Mk 13:28 SUV

Kwa mtini jifunzeni mfano; tawi lake liishapo kuwa laini, na kuchanua majani, mwatambua ya kuwa wakati wa mavuno ni karibu

Mk 13:29 SUV

nanyi kadhalika, myaonapo mambo hayo yanaanza, tambueni ya kuwa yu karibu milangoni.

Mk 13:30 SUV

Amin, nawaambieni, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatimie.

Mk 13:31 SUV

Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe.