YouVersion Logo
Search Icon

Mk 12:13, 14, 15, 16, 17, 18, 19, 20, 21, 22, 23, 24, 25, 26, 27, 28, 29, 30, 31, 32, 33, 34

Mk 12:13 SUV

Wakatuma kwake baadhi ya Mafarisayo na Maherodi, ili wamnase kwa maneno.

Mk 12:14 SUV

Hata walipofika walimwambia, Mwalimu, twajua ya kuwa wewe u mtu wa kweli, wala hujali cheo cha mtu; kwa maana hutazami sura za watu; lakini katika kweli waifundisha njia ya Mungu. Je! Ni halali kumpa Kaisari kodi au siyo?

Mk 12:15 SUV

Tumpe, tusimpe? Naye, akijua unafiki wao, akawaambia, Mbona mmenijaribu? Nileteeni dinari niione.

Mk 12:16 SUV

Wakaileta. Akawaambia, Ni ya nani sanamu hii na anwani hii? Wakamwambia, Ni ya Kaisari.

Mk 12:17 SUV

Yesu akajibu, akawaambia, Mpeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na yaliyo ya Mungu mpeni Mungu. Wakamstaajabia sana.

Mk 12:18 SUV

Kisha Masadukayo, watu wasemao ya kwamba hakuna kiyama, wakamwendea, wakamwuliza na kusema

Mk 12:19 SUV

Mwalimu, Musa alituandikia ya kwamba ndugu ya mtu akifa, akamwacha mkewe wala hana mtoto, ndugu yake amtwae yule mkewe akampatie ndugu yake mzao.

Mk 12:20 SUV

Basi kulikuwa na ndugu saba, wa kwanza akatwaa mke, akafa, asiache mzao.

Mk 12:21 SUV

Wa pili naye akamtwaa akafa, wala yeye hakuacha mzao. Na wa tatu kadhalika

Mk 12:22 SUV

hata na wote saba, wasiache mzao. Mwisho wa wote yule mwanamke akafa naye.

Mk 12:23 SUV

Basi, katika kiyama atakuwa mke wa yupi katika hao? Maana wote saba walikuwa naye.

Mk 12:24 SUV

Yesu akajibu, akawaambia, Je! Hampotei kwa sababu hii, kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa Mungu?

Mk 12:25 SUV

Kwa maana watakapofufuka katika wafu, hawaoi wala hawaolewi, bali huwa kama malaika walioko mbinguni.

Mk 12:26 SUV

Na kwa habari ya wafu ya kwamba wafufuliwa, hamjasoma katika kitabu cha Musa, Sura ya Kijiti, jinsi Mungu alivyomwambia, akisema, Mimi ni Mungu wa Ibrahimu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo?

Mk 12:27 SUV

Yeye si Mungu wa wafu, bali wa walio hai. Hivyo mwapotea sana.

Mk 12:28 SUV

Na mmojawapo wa waandishi akafika, akawasikia wakisemezana naye, akatambua ya kuwa amewajibu vema, akamwuliza, Katika amri zote ni ipi iliyo ya kwanza?

Mk 12:29 SUV

Yesu akamjibu, Ya kwanza ndiyo hii, Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja

Mk 12:30 SUV

nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote.

Mk 12:31 SUV

Na ya pili ndiyo hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi.

Mk 12:32 SUV

Yule mwandishi akamwambia, Hakika, Mwalimu, umesema vema ya kwamba Mungu ni mmoja, wala hakuna mwingine ila yeye

Mk 12:33 SUV

na kumpenda yeye kwa moyo wote, na kwa ufahamu wote, na kwa nguvu zote, na kumpenda jirani kama nafsi yako, kwafaa kuliko sadaka nzima za kuteketezwa na dhahibu zote pia.

Mk 12:34 SUV

Naye Yesu, alipoona kwamba amejibu kwa busara, alimwambia, Wewe hu mbali na ufalme wa Mungu. Wala hakuthubutu mtu kumsaili neno tena tokea hapo.