YouVersion Logo
Search Icon

Mk 12:1, 2, 3, 4, 5, 6, 7, 8, 9, 10, 11

Mk 12:1 SUV

Akaanza kusema nao kwa mifano; Mtu mmoja alipanda shamba la mizabibu, akazungusha ugo, akachimba shimo la shinikizo, akajenga mnara, akapangisha wakulima, akasafiri.

Mk 12:2 SUV

Hata kwa wakati wake akatuma mtumwa kwa wale wakulima, ili apokee kwa wakulima katika matunda ya mizabibu.

Mk 12:3 SUV

Wakamtwaa, wakampiga, wakamtoa nje, hana kitu.

Mk 12:4 SUV

Akatuma tena kwao mtumwa mwingine, na huyo wakamtia jeraha za kichwa, wakamfanyia jeuri.

Mk 12:5 SUV

Akamtuma mwingine, huyo wakamwua; na wengine wengi, hawa wakiwapiga na hawa wakiwaua.

Mk 12:6 SUV

Basi alikuwa na mmoja bado, mwana mpendwa wake; huyu naye akamtuma kwao mwisho, akisema, Watamstahi mwanangu.

Mk 12:7 SUV

Lakini wale wakulima wakasemezana, Huyu ni mrithi; haya, na tumwue, na urithi utakuwa wetu.

Mk 12:8 SUV

Wakamkamata, wakamwua, wakamtupa nje ya shamba la mizabibu.

Mk 12:9 SUV

basi atafanyaje yule bwana wa shamba la mizabibu? Atakuja na kuwaangamiza wale wakulima, na lile shamba la mizabibu atawapa wengine.

Mk 12:10 SUV

Hata andiko hili hamjalisoma, Jiwe walilolikataa waashi, Hilo limekuwa jiwe kuu la pembeni.

Mk 12:11 SUV

Neno hili limetoka kwa Bwana, Nalo ni ajabu machoni petu?