YouVersion Logo
Search Icon

Mk 11:27, 28, 29, 30, 31, 32

Mk 11:27 SUV

Wakafika Yerusalemu tena; hata alipokuwa akitembea hekaluni, walimwendea wakuu wa makuhani, na waandishi, na wazee

Mk 11:28 SUV

wakamwambia, Ni kwa mamlaka gani unatenda mambo haya? Naye ni nani aliyekupa mamlaka hii uyatende haya?

Mk 11:29 SUV

Yesu akawaambia, Nitawauliza neno moja, nanyi mnijibu, kisha nitawaambia ni kwa mamlaka gani nayatenda haya.

Mk 11:30 SUV

Ubatizo wa Yohana ulitoka mbinguni, au kwa wanadamu? Nijibuni.

Mk 11:31 SUV

Wakasemezana wao kwa wao, wakisema, Kama tukisema, Ulitoka mbinguni, atasema, Mbona, basi, hamkumwamini?

Mk 11:32 SUV

Ila tukisema, Ulitoka kwa wanadamu, – waliogopa watu; maana watu wote walimwona Yohana kuwa nabii halisi.