YouVersion Logo
Search Icon

Mt 7:8, 9, 10, 11, 12, 13, 14, 15, 16, 17, 18, 19, 20, 21, 22, 23, 24, 25, 26, 27, 28, 29

Mt 7:8 SUV

kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa.

Mt 7:9 SUV

Au kuna mtu yupi kwenu, ambaye, mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe?

Mt 7:10 SUV

Au akiomba samaki, atampa nyoka?

Mt 7:11 SUV

Basi ikiwa ninyi, mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema wao wamwombao?

Mt 7:12 SUV

Basi yo yote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo torati na manabii.

Mt 7:13 SUV

Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo.

Mt 7:14 SUV

Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.

Mt 7:15 SUV

Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali.

Mt 7:16 SUV

Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti?

Mt 7:17 SUV

Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya.

Mt 7:18 SUV

Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri.

Mt 7:19 SUV

Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni.

Mt 7:20 SUV

Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua.

Mt 7:21 SUV

Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.

Mt 7:22 SUV

Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?

Mt 7:23 SUV

Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.

Mt 7:24 SUV

Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba

Mt 7:25 SUV

mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba.

Mt 7:26 SUV

Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga

Mt 7:27 SUV

mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; nalo anguko lake likawa kubwa.

Mt 7:28 SUV

Ikawa, Yesu alipoyamaliza maneno hayo, makutano walishangaa mno kwa mafundisho yake

Mt 7:29 SUV

kwa maana alikuwa akiwafundisha kama mtu mwenye amri, wala si kama waandishi wao.