Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mt 21

21
Yesu Aingia Yerusalemu kwa Shangwe
1 # Mk 11:1-10; Lk 19:29-38; Yn 12:12-19 Hata walipokaribia Yerusalemu, na kufika Bethfage, katika mlima wa Mizeituni, ndipo Yesu alipotuma wanafunzi wawili akiwaambia, 2Enendeni mpaka kijiji kile kinachowakabili, na mara mtaona punda amefungwa, na mwana-punda pamoja naye; wafungueni mniletee. 3#Mt 26:18Na kama mtu akiwaambia neno, semeni, Bwana anawahitaji; na mara huyo atawapeleka. 4Haya yote yamekuwa, ili litimie neno lililonenwa na nabii, akisema,
5 # Zek 9:9; Isa 62:11 Mwambieni binti Sayuni
Tazama, mfalme wako anakuja kwako,
Mpole, naye amepanda punda,
Na mwana-punda, mtoto wa punda.
6Wale wanafunzi wakaenda zao, wakafanya kama Yesu alivyowaamuru, 7wakamleta yule punda na mwana-punda, wakaweka nguo zao juu yao, naye akaketi juu yake. 8#2 Fal 9:13Watu wengi katika ule mkutano wakatandaza nguo zao njiani; na wengine wakakata matawi ya miti, wakayatandaza njiani. 9#Zab 118:25-26; 2 Sam 14:4Na makutano waliotangulia, na wale waliofuata, wakapaza sauti, wakisema, Hosana, Mwana wa Daudi; ndiye mbarikiwa, yeye ajaye kwa jina la Bwana; Hosana juu mbinguni. 10Hata alipoingia Yerusalemu, mji wote ukataharuki, watu wakisema, Ni nani huyu? 11#Mt 21:46Makutano wakasema, Huyu ni yule nabii, Yesu, wa Nazareti ya Galilaya.
Yesu Atakasa Hekalu
12 # Mk 11:11-24; Lk 19:45-48; Yn 2:14-16 Yesu akaingia ndani ya hekalu, akawafukuza wote waliokuwa wakiuza na kununua hekaluni, akazipindua meza za wabadili fedha, na viti vyao waliokuwa wakiuza njiwa; 13#Isa 56:7; Yer 7:11akawaambia, Imeandikwa, Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala; bali ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang’anyi. 14Na vipofu na viwete wakamwendea mle hekaluni, akawaponya. 15#Zab 118:25Lakini wakuu wa makuhani na waandishi walipoyaona maajabu aliyoyafanya, na watoto waliopaza sauti zao hekaluni, wakisema, Hosana, Mwana wa Daudi! Walikasirika, 16#Zab 8:3wakamwambia, Wasikia hawa wasemavyo? Yesu akawaambia, Naam; hamkupata kusoma, Kwa vinywa vya watoto wachanga na wanyonyao umekamilisha sifa? 17Akawaacha, akatoka nje ya mji mpaka Bethania, akalala huko.
Yesu Aulaani Mtini
18Hata asubuhi alipokuwa akienda mjini, aliona njaa. 19#Lk 13:6Akaona mtini mmoja kando ya njia, akauendea, asione kitu juu yake ila majani tu; akauambia, Yasipatikane matunda kwako tangu leo hata milele. Mtini ukanyauka mara. 20Wanafunzi walipoona, walistaajabu, wakisema, Jinsi gani mtini umenyauka mara? 21#Mt 17:20; 1 Kor 13:2Yesu akajibu, akawaambia, Amin, nawaambia Mkiwa na imani, msipokuwa na shaka, mtafanya si hilo la mtini tu, lakini hata mkiuambia mlima huu, Ng’oka, ukatupwe baharini, litatendeka. 22Na yo yote mtakayoyaomba katika sala mkiamini, mtapokea.
Swali kuhusu Mamlaka ya Yesu
23 # Mk 11:27-33; Lk 20:1-8 # Yn 2:18 Hata alipokwisha kuingia hekaluni, wakuu wa makuhani na wazee wa watu wakamwendea alipokuwa akifundisha, wakasema, Ni kwa amri gani unatenda mambo haya? Naye ni nani aliyekupa amri hii? 24Yesu akajibu akawaambia, Na mimi nitawauliza neno moja; ambalo mkinijibu, nami nitawaambia ni kwa amri gani ninatenda haya. 25Ubatizo wa Yohana ulitoka wapi? Ulitoka mbinguni, au kwa wanadamu? Wakahojiana wao kwa wao, wakisema, Tukisema, Ulitoka mbinguni, atatuambia, Mbona basi hamkumwamini? 26#Mt 14:5Na tukisema, Ulitoka kwa wanadamu, twaogopa mkutano; maana watu wote wamwona Yohana kuwa ni nabii. 27Wakamjibu Yesu wakasema, Hatujui. Naye akawaambia, Wala mimi siwaambii ninyi ni kwa amri gani ninatenda haya.
Mfano kuhusu Wana Wawili
28Lakini mwaonaje? Mtu mmoja alikuwa na wana wawili; akamwendea yule wa kwanza, akasema, Mwanangu, leo nenda kafanye kazi katika shamba la mizabibu. 29#Mt 7:21Akajibu akasema, Naenda, Bwana; asiende. 30Akamwendea yule wa pili, akasema vile vile. Naye akajibu akasema, Sitaki; baadaye akatubu, akaenda. 31#Lk 18:14Je! Katika hao wawili ni yupi aliyefanya mapenzi ya babaye? Wakamwambia, Ni yule wa pili. Basi Yesu akawaambia, Amin nawaambia, watoza ushuru na makahaba wanatangulia mbele yenu kuingia katika ufalme wa Mungu. 32#Lk 3:12; 7:29-30Kwa sababu Yohana alikuja kwenu kwa njia ya haki, ninyi msimwamini; lakini watoza ushuru na makahaba walimwamini, nanyi hata mlipoona, hamkutubu baadaye, ili kumwamini.
Mfano wa Wakulima Waovu
33 # Mk 12:1-12; Lk 20:9-19 # Isa 5:1-2; Mt 25:14 Sikilizeni mfano mwingine. Kulikuwa na mtu mwenye nyumba, naye alipanda shamba la mizabibu, akalizungusha ugo, akachimba shimo la shinikizo ndani yake, akajenga mnara, akapangisha wakulima, akasafiri. 34Wakati wa matunda ulipokuwa karibu, akawatuma watumwa wake kwa wale wakulima, wapokee matunda yake. 35Wale wakulima wakawakamata watumwa wake, huyu wakampiga, na huyu wakamwua, na huyu wakampiga kwa mawe. 36Akawatuma tena watumwa wengine wengi kuliko wa kwanza wakawatenda vile vile. 37Mwishowe akamtuma mwanawe kwao, akisema, Watamstahi mwanangu. 38#Mt 27:18Lakini wale wakulima walipomwona yule mwana, wakasemezana wao kwa wao, Huyu ni mrithi; haya na tumwue, tuutwae urithi wake. 39Wakamkamata, wakamtupa nje ya shamba la mizabibu, wakamwua. 40Basi atakapokuja yule bwana wa shamba la mizabibu, atawatendaje wale wakulima? 41Wakamwambia, Atawaangamiza vibaya wale wabaya; na shamba la mizabibu atawapangisha wakulima wengine, watakaomlipa matunda kwa wakati wake. 42#Zab 118:22-23; Mdo 4:11; Rum 9:33; 1 Pet 2:6-8Yesu akawaambia, Hamkupata kusoma katika maandiko,
Jiwe walilolikataa waashi,
Hilo limekuwa jiwe kuu la pembeni;
Neno hili limetoka kwa Bwana,
Nalo ni ajabu machoni petu?
43Kwa sababu hiyo nawaambia, Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, nao watapewa taifa lingine lenye kuzaa matunda yake. 44#Dan 2:34,35,44,45Naye aangukaye juu ya jiwe hilo atavunjika-vunjika; naye ye yote ambaye litamwangukia, litamsaga tikitiki. 45Wakuu wa makuhani na Mafarisayo, waliposikia mifano yake, walitambua ya kuwa anawanenea wao. 46Nao walipotafuta kumkamata, waliwaogopa makutano, kwa maana wao walimwona kuwa nabii.

Iliyochaguliwa sasa

Mt 21: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia