YouVersion Logo
Search Icon

Mt 2:13, 14, 15, 16, 17, 18, 19, 20, 21, 22, 23

Mt 2:13 SUV

Na hao walipokwisha kwenda zao, tazama, malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto, akasema, Ondoka, umchukue mtoto na mama yake, ukimbilie Misri, ukae huko hata nikuambie; kwa maana Herode anataka kumtafuta mtoto amwangamize.

Mt 2:14 SUV

Akaondoka akamchukua mtoto na mama yake usiku, akaenda zake Misri

Mt 2:15 SUV

akakaa huko hata alipokufa Herode; ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii, akisema, Kutoka Misri nalimwita mwanangu.

Mt 2:16 SUV

Ndipo Herode, alipoona ya kuwa amedhihakiwa na wale mamajusi, alighadhabika sana, akatuma watu akawaua watoto wote wanaume waliokuwako huko Bethlehemu na viungani mwake mwote, tangu wenye miaka miwili na waliopungua, kwa muda ule aliouhakikisha kwa wale mamajusi.

Mt 2:17 SUV

Ndipo lilipotimia neno lililonenwa na nabii Yeremia, akisema

Mt 2:18 SUV

Sauti ilisikiwa Rama, Kilio, na maombolezo mengi, Raheli akiwalilia watoto wake, Asikubali kufarijiwa, kwa kuwa hawako.

Mt 2:19 SUV

Hata alipofariki Herode, tazama, malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto huko Misri

Mt 2:20 SUV

akasema, Ondoka, umchukue mtoto na mamaye, ushike njia kwenda nchi ya Israeli; kwa maana wamekufa walioitafuta roho ya mtoto.

Mt 2:21 SUV

Akaondoka akamchukua mtoto na mamaye, akafika nchi ya Israeli.

Mt 2:22 SUV

Lakini aliposikia ya kwamba Arkelao anamiliki huko Uyahudi mahali pa Herode babaye, aliogopa kwenda huko; naye akiisha kuonywa katika ndoto, akasafiri pande za Galilaya

Mt 2:23 SUV

akaenda, akakaa katika mji ulioitwa Nazareti; ili litimie neno lililonenwa na manabii, Ataitwa Mnazorayo.

Video for Mt 2:13-23

Free Reading Plans and Devotionals related to Mt 2:13, 14, 15, 16, 17, 18, 19, 20, 21, 22, 23