YouVersion Logo
Search Icon

Mt 15:29, 30, 31, 32, 33, 34, 35, 36, 37, 38

Mt 15:29 SUV

Yesu akaondoka huko, akafika kando ya bahari ya Galilaya; akapanda mlimani, akaketi huko.

Mt 15:30 SUV

Wakamwendea makutano mengi wakimletea viwete, vipofu, mabubu, vilema, na wengine wengi, wakawaweka miguuni pake; akawaponya

Mt 15:31 SUV

hata ule mkutano wakastaajabu, walipowaona mabubu wanasema, vilema wanakuwa wazima, viwete wanakwenda, na vipofu wanaona; wakamtukuza Mungu wa Israeli.

Mt 15:32 SUV

Yesu akawaita wanafunzi wake, akasema, Nawahurumia mkutano, kwa kuwa yapata siku tatu wamekaa pamoja nami, wala hawana kitu cha kula, tena kuwaaga wakifunga sipendi, wasije wakazimia njiani.

Mt 15:33 SUV

Wanafunzi wake wakamwambia, Tupate wapi mikate mingi hapa nyikani, hata kushibisha mkutano mkuu namna hii?

Mt 15:34 SUV

Yesu akawaambia, Mnayo mikate mingapi? Wakasema, Saba, na visamaki vichache.

Mt 15:35 SUV

Akawaagiza mkutano waketi chini

Mt 15:36 SUV

akaitwaa ile mikate saba na vile visamaki, akashukuru akavimega, akawapa wanafunzi wake, nao wanafunzi wakawapa makutano.

Mt 15:37 SUV

Wakala wote wakashiba; wakayaokota masazo ya vipande vya mikate makanda saba, yamejaa.

Mt 15:38 SUV

Nao waliokula walikuwa wanaume elfu nne, bila wanawake na watoto.