Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mt 11:25-27

Mt 11:25-27 SUV

Wakati ule Yesu akajibu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga. Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyopendeza mbele zako. Akasema, Nimekabidhiwa vyote na baba yangu; wala hakuna amjuaye Mwana, ila Baba; wala hakuna amjuaye Baba, ila Mwana, na ye yote ambaye Mwana apenda kumfunulia.

Soma Mt 11

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Mt 11:25-27