Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mal 4

4
Siku Kuu ya Bwana
1Kwa maana, angalieni, siku ile inakuja, inawaka kama tanuru; na watu wote wenye kiburi, nao wote watendao uovu, watakuwa makapi; na siku ile inayokuja itawateketeza, asema BWANA wa majeshi; hata haitawaachia shina wala tawi. 2#Lk 1:78; Efe 5:14; 2 Pet 1:19Lakini kwenu ninyi mnaolicha jina langu, jua la haki litawazukia, lenye kuponya katika mbawa zake; nanyi mtatoka nje, na kucheza-cheza kama ndama wa mazizini. 3#Mik 7:10Nanyi mtawakanyaga waovu; maana watakuwa majivu chini ya nyayo za miguu yenu; katika siku ile niifanyayo, asema BWANA wa majeshi.
4 # Kum 4:10 Ikumbukeni torati ya Musa, mtumishi wangu, niliyomwamuru huko Horebu kwa ajili ya Israeli wote, naam, amri na hukumu. 5#Yoe 2:31; Mt 11:14; 17:10-13; Mk 9:11-13; Lk 1:17; Yn 1:21Angalieni, nitawapelekea Eliya nabii, kabla haijaja siku ile ya BWANA, iliyo kuu na kuogofya. 6#Lk 1:17; Dan 9:26; Lk 19:27,43; 21:20; Mk 13:14Naye ataigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto wao, na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, ili nisije nikaipiga dunia kwa laana.

Iliyochaguliwa sasa

Mal 4: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia