Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mal 1

1
Israeli Wapendwa kuliko Edomu
1Ufunuo wa neno la BWANA kwa Israeli kwa mkono wa Malaki 2#Mwa 25:23; 28:13; Rum 9:13#Isa 34:5-17; 63:1-6; Yer 49:7-22; Eze 25:12-14; 35:1-15; Amo 1:11-12; Oba 1-14Nimewapenda ninyi, asema BWANA. Lakini ninyi mwasema, Umetupendaje? Je! Esau siye ndugu yake Yakobo? Asema BWANA; ila nimempenda Yakobo; 3bali Esau nimemchukia na kuifanya milima yake kuwa ukiwa, na urithi wake nimewapa mbweha wa nyikani. 4Ijapokuwa Edomu asema, Tumepondwa-pondwa, lakini tutarudi na kupajenga mahali palipoachwa hali ya ukiwa; BWANA wa majeshi asema hivi, Wao watajenga, bali mimi nitaangusha; na watu watawaita, Mpaka wa uovu, na, Watu ambao BWANA anawaghadhabikia milele. 5#Zab 35:27; 83:18Na macho yenu ninyi yataona, nanyi mtasema, BWANA ndiye mkuu kupita mpaka wa Israeli.
Uoza wa Ukuhani
6 # Kut 20:12; Kum 5:16; Mt 15:4; Efe 6:2; Lk 18:20; 6:46 Mwana humheshimu baba yake, na mtumishi humcha bwana wake; basi, kama mimi ni baba yenu, heshima yangu iko wapi? Na kama mimi ni bwana wenu, kicho changu ki wapi? BWANA wa majeshi awauliza ninyi, enyi makuhani, mnaolidharau jina langu. Nanyi mwasema, Tumelidharau jina lako kwa jinsi gani? 7#Eze 41:22Mnatoa chakula kilichotiwa unajisi juu ya madhabahu yangu Nanyi mwasema, Sisi tumekutia unajisi kwa jinsi gani? Kwa sababu mwasema, Meza ya BWANA ni kitu cha kudharauliwa. 8#Ayu 42:8; Kum 15:21Tena mtoapo sadaka aliye kipofu, si vibaya? Na mtoapo sadaka walio vilema na wagonjwa, si vibaya? Haya! Mtolee liwali wako; je! Atakuwa radhi nawe? Au atakukubali nafsi yako? Asema BWANA wa majeshi. 9#Hos 13:9Na sasa, nawasihi, ombeni fadhili za Mungu, ili atupe neema; ikiwa jambo hili limetoka katika mikono yenu; je! Atawakubali nafsi zenu? Asema BWANA wa majeshi. 10#1 Kor 9:13; Flp 3:18,19; Isa 1:11Laiti angekuwapo kwenu mtu mmoja wa kuifunga milango; msije mkawasha moto bure madhabahuni pangu! Sina furaha kwenu, asema BWANA wa majeshi, wala sitakubali dhabihu yo yote mikononi mwenu. 11#Isa 59:19; 66:19; Yn 4:21; 1 Tim 2:8; Ufu 8:3Kwa maana tokea maawio ya jua hata machweo yake jina langu ni kuu katika Mataifa; na katika kila mahali unatolewa uvumba na dhabihu safi kwa jina langu; maana jina langu ni kuu katika Mataifa, asema BWANA wa majeshi. 12Lakini ninyi mnalitia unajisi, kwa kuwa mwasema, Meza ya BWANA imetiwa unajisi; na matunda yake, yaani, nyama yake, hudharauliwa. 13#Law 22:20; Isa 1:12Tena mwasema, Tazama, jambo hili linatuchokesha namna gani! Nanyi mmelidharau, asema BWANA wa majeshi; nanyi mmeleta kitu kilichopatikana kwa udhalimu, na kilema, na kilicho kigonjwa; ndivyo mnavyoleta sadaka; je! Niikubali hii mikononi mwenu? Asema BWANA. 14#Mdo 5:1Lakini na alaaniwe mtu mwenye kudanganya, ambaye katika kundi lake ana mume, akaweka nadhiri, ila amtolea Bwana kitu kilicho na kilema; kwa maana mimi ni Mfalme mkuu, asema BWANA wa majeshi, na jina langu latisha katika Mataifa.

Iliyochaguliwa sasa

Mal 1: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia