YouVersion Logo
Search Icon

Lk 9:1, 2, 3, 4, 5, 6, 7, 8

Lk 9:1 SUV

Akawaita wale Thenashara, akawapa uwezo na mamlaka juu ya pepo wote na kuponya maradhi.

Lk 9:2 SUV

Akawatuma wautangaze ufalme wa Mungu, na kupoza wagonjwa.

Lk 9:3 SUV

Akawaambia, Msichukue kitu kwa safari yenu, fimbo, wala mkoba, wala mkate, wala fedha, wala mmoja wenu asiwe na kanzu mbili.

Lk 9:4 SUV

Na nyumba yo yote mtakayoingia kaeni humo, mpaka mtoke mjini.

Lk 9:5 SUV

Na wale wasiowakaribisha, mtokapo katika mji huo, yakung’uteni hata mavumbi ya miguuni mwenu, kuwa ushuhuda juu yao.

Lk 9:6 SUV

Wakaenda, wakazunguka katika vijiji, wakihubiri injili, na kupoza watu kila mahali.

Lk 9:7 SUV

Na Herode mfalme akasikia habari za yote yaliyotendeka, akafadhaika kwa sababu watu wengine walisema ya kwamba Yohana amefufuka katika wafu

Lk 9:8 SUV

na wengine ya kwamba Eliya ametokea, na wengine ya kwamba mmojawapo wa manabii wa kale amefufuka.