Lk 23:50, 51, 52, 53, 54, 55
Lk 23:50 SUV
Na tazama, akatoka mtu mmoja, jina lake Yusufu, ambaye ni mtu wa baraza, mtu mwema, mwenye haki
Lk 23:51 SUV
(wala hakulikubali shauri na tendo lao), naye ni mtu wa Arimathaya, mji mmoja wa Wayahudi, tena anautazamia ufalme wa Mungu
Lk 23:53 SUV
Akaushusha, akauzinga sanda ya kitani, akauweka katika kaburi lililochongwa mwambani, ambalo hajalazwa mtu bado ndani yake.
Lk 23:54 SUV
Na siku ile ilikuwa siku ya Maandalio, na sabato ikaanza kuingia.
Lk 23:55 SUV
Na wale wanawake waliokuja naye toka Galilaya walifuata, wakaliona kaburi, na jinsi mwili wake ulivyowekwa.