YouVersion Logo
Search Icon

Lk 23:1, 2, 3, 4, 5, 6, 7, 8, 9, 10, 11, 12, 13, 14, 15, 16, 17, 18, 19, 20, 21, 22, 24, 25

Lk 23:1 SUV

Wakasimama mkutano wote, wakampeleka kwa Pilato.

Lk 23:2 SUV

Wakaanza kumshitaki, wakisema, Tumemwona huyu akipotosha taifa letu, na kuwazuia watu wasimpe Kaisari kodi, akisema kwamba yeye mwenyewe ni Kristo, mfalme.

Lk 23:3 SUV

Pilato akamwuliza, akisema, Wewe ndiwe mfalme wa Wayahudi? Akajibu akamwambia, Wewe wasema.

Lk 23:4 SUV

Pilato akawaambia wakuu wa makuhani na makutano, Sioni neno lililo ovu katika mtu huyu.

Lk 23:5 SUV

Nao walikaza sana, wakisema, Huwataharakisha watu, akifundisha katika Uyahudi yote, tokea Galilaya mpaka huku.

Lk 23:6 SUV

Pilato aliposikia hayo aliuliza kama huyu ni mtu wa Galilaya.

Lk 23:7 SUV

Na alipopata habari ya kuwa yu chini ya mamlaka ya Herode, alimpeleka kwa Herode, kwa kuwa yeye naye alikuwapo Yerusalemu siku zile.

Lk 23:8 SUV

Na Herode alipomwona Yesu alifurahi sana, kwa sababu alikuwa akitaka sana kumwona tangu siku nyingi, maana amesikia habari zake, akataraji kuona ishara iliyofanywa na yeye.

Lk 23:9 SUV

Akamwuliza maneno mengi, yeye asimjibu lo lote.

Lk 23:10 SUV

Wakuu wa makuhani na waandishi wakasimama wakamshitaki kwa nguvu sana.

Lk 23:11 SUV

Basi Herode akamfanya duni, pamoja na askari zake, akamdhihaki, na kumvika mavazi mazuri; kisha akamrudisha kwa Pilato.

Lk 23:12 SUV

Basi siku ile ile Herode na Pilato walipatana kwa urafiki kwa maana hapo kwanza walikuwa na uadui wao kwa wao.

Lk 23:13 SUV

Na Pilato akawakutanisha wakuu wa makuhani, na wakubwa, na watu

Lk 23:14 SUV

akawaambia, Mtu huyu mmemleta kwangu kana kwamba anapotosha watu; nami, tazama, nimeamua mambo yake mbele yenu, ila sikuona kwake kosa lo lote katika mambo hayo mliyomshitaki

Lk 23:15 SUV

wala hata Herode, kwa maana amemrudisha kwetu; basi tazama, hakuna neno lo lote alilolitenda lipasalo kufa.

Lk 23:16 SUV

Kwa hiyo nitamrudi, kisha nitamfungua. [

Lk 23:17 SUV

Maana ilimlazimu kuwafungulia mfungwa mmoja wakati wa sikukuu.]

Lk 23:18 SUV

Wakapiga kelele wote pamoja, wakisema, Mwondoe huyu, utufungulie Baraba.

Lk 23:19 SUV

Naye ni mtu aliyetupwa gerezani kwa ajili ya fitina iliyotokea mjini, na kwa uuaji

Lk 23:20 SUV

Basi Pilato alisema nao mara ya pili, kwa vile alivyotaka kumfungua Yesu.

Lk 23:21 SUV

Lakini wakapiga kelele, wakisema, Msulibishe. Msulibishe.

Lk 23:22 SUV

Akawaambia mara ya tatu, Kwa sababu gani? Huyu ametenda uovu gani? Sikuona kwake hata neno lipasalo kufa. Basi nikiisha kumrudi nitamfungua.

Lk 23:24 SUV

Pilato akahukumu kwamba haja yao ifanyike.

Lk 23:25 SUV

Akamfungua yule aliyetupwa gerezani kwa ajili ya fitina na uuaji, yule waliyemtaka, akamtoa Yesu wamfanyie watakavyo.