YouVersion Logo
Search Icon

Lk 22:66, 67, 68, 69, 70

Lk 22:66 SUV

Hata kulipokucha, walikutanika jamii ya wazee, na wakuu wa makuhani, na waandishi, wakamleta katika baraza yao, wakisema

Lk 22:67 SUV

Kama wewe ndiwe Kristo, tuambie. Akawaambia, Nijapowaambia, hamtasadiki kabisa.

Lk 22:68 SUV

Tena, nikiwauliza, hamtajibu.

Lk 22:69 SUV

Lakini tangu sasa Mwana wa Adamu atakuwa ameketi upande wa kuume wa Mungu Mwenyezi.

Lk 22:70 SUV

Wakasema wote, Basi, wewe ndiwe Mwana wa Mungu? Akawaambia, Ninyi mwasema kwamba mimi ndiye.