YouVersion Logo
Search Icon

Lk 14:25, 26, 27, 28, 29, 30, 31, 32, 33, 34

Lk 14:25 SUV

Makutano mengi walipokuwa wakifuatana naye, aligeuka, akawaambia

Lk 14:26 SUV

Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake waume na wake; naam, na hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.

Lk 14:27 SUV

Mtu ye yote asiyeuchukua msalaba wake na kuja nyuma yangu, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.

Lk 14:28 SUV

Maana ni nani katika ninyi, kama akitaka kujenga mnara, asiyeketi kwanza na kuhesabu gharama, kwamba anavyo vya kuumalizia?

Lk 14:29 SUV

Asije akashindwa kuumaliza baada ya kuupiga msingi, watu wote waonao wakaanza kumdhihaki

Lk 14:30 SUV

wakisema, Mtu huyu alianza kujenga, akawa hana nguvu za kumaliza.

Lk 14:31 SUV

Au kuna mfalme gani, akitaka kwenda kupigana na mfalme mwingine, asiyeketi kwanza na kufanya shauri, kwamba yeye pamoja na watu elfu kumi ataweza kukutana na yule anayekuja juu yake na watu elfu ishirini?

Lk 14:32 SUV

Na kama akiona hawezi, hutuma ujumbe kutaka sharti za amani, mtu yule akali mbali.

Lk 14:33 SUV

Basi, kadhalika kila mmoja wenu asiyeacha vyote alivyo navyo, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.

Lk 14:34 SUV

Chumvi ni kitu chema; lakini chumvi ikiwa imeharibika, itiwe nini ikolee?