Law 20
20
Adhabu ya Kukiuka Maadili ya Utakatifu
1Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia, 2#2 Fal 17:17; 23:10; 2 Nya 33:6Tena uwaambie wana wa Israeli, Mtu awaye yote miongoni mwa wana wa Israeli, au miongoni mwa wageni waketio katika Israeli, atakayetoa katika kizazi chake na kumpa Moleki, sharti atauawa; wenyeji wa nchi watampiga kwa mawe. 3#Eze 5:11; 23:38,39; Hes 19:20Mimi nami nitamkazia uso wangu mtu huyo, nami nitamkatilia mbali na watu wake; kwa kuwa ametoa katika kizazi chake na kumpa Moleki, ili kupatia unajisi patakatifu pangu, na kulinajisi jina langu takatifu. 4Tena kama wenyeji wa nchi wakimfumbia macho mtu huyo kwa njia yo yote, hapo atoapo katika kizazi chake na kumpa Moleki, wasimwue; 5#Kut 20:5; Law 17:7ndipo mimi nitamkazia uso wangu mtu huyo, na jamaa zake, nami nitamkatilia mbali, na hao wote wamwandamao katika uzinifu, ili kufanya uzinifu pamoja na Moleki, watengwe mbali na watu wao.
6 #
Law 19:31; 2 Fal 23:24 Na mtu yule atakayewaendea wenye pepo, na wachawi, ili kuzini pamoja nao, nitakaza uso wangu juu ya mtu yule, nitamtenga na watu wake. 7#Kut 22:31; Mt 5:48; Efe 1:4; Kol 3:12; 1 The 5:23; 1 Pet 1:16Jitakaseni basi, iweni watakatifu, kwa kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wenu. 8#Kut 31:13; Eze 37:28Nanyi zishikeni sheria zangu, na kuzitenda; Mimi ndimi BWANA niwatakasaye ninyi. 9#Kut 21:17; Mt 15:4; Mk 7:10; Kum 27:16; Mit 20:20; 2 Sam 1:16; 1 Fal 2:32Kwa maana kila mtu amlaaniye baba yake au mama yake hakika atauawa, amemlaani baba yake na mama yake; damu yake itakuwa juu yake. 10#Kut 20:14; Law 18:20; Kum 5:18; 22:22; Yer 29:23; Yn 8:4,5; 1 Kor 6:9; Ebr 13:4Na mtu aziniye na mke wa mtu mwingine, naam, yeye aziniye na mke wa jirani yake, mtu mume aziniye, na mwanamke aziniye, hakika watauawa. 11#Law 18:8; Kum 22:30; 27:20,23Na mtu mume atakayelala pamoja na mke wa baba yake amefunua utupu wa baba yake; wote wawili hakika watauawa; damu yao itakuwa juu yao. 12#Law 18:15Na mtu mume akilala na mkwewe mwanamke wote wawili hakika watauawa; wamefanya yaliyo uchafuko; damu yao itakuwa juu yao. 13#Law 18:22; Mwa 19:5; Rum 1:25,32Tena mtu mume akilala pamoja na mtu mume, kama alalavyo na mtu mke, wote wawili wamefanya machukizo; hakika watauawa; damu yao itakuwa juu yao. 14#Law 18:17; Kum 27:23Tena mtu mume akimwoa mke pamoja na mama yake, ni uovu mkuu; watachomwa moto, yeye mume na hao wanawake pia; ili kwamba usiwe uovu kati yenu. 15#Kut 22:19; Law 18:23; Kum 27:21Tena mtu mume akilala na mnyama, hakika atauawa; nanyi mtamwua huyo mnyama. 16Tena mwanamke akimkaribia mnyama ye yote, na kulala pamoja naye, mtamwua huyo mwanamke, na mnyama pia; hakika watauawa; damu yao itakuwa ni juu yao. 17#Law 18:9; Kum 27:22; Mwa 20:12Tena mtu mume akimwoa umbu lake, binti ya baba yake, au binti ya mama yake, na kuuona utupu wake, na huyo mwanamke kauona utupu wake huyo mume; ni jambo la aibu; watakatiliwa mbali mbele ya macho ya wana wa watu wao; amefunua utupu wa umbu lake; naye atauchukua uovu wake. 18#Law 18:19; 15:24Tena mtu mume akilala na mwanamke aliye na ugonjwa wake, na kufunua utupu wake; amelifunua jito la damu yake, naye mwanamke amefunua jito la damu yake; wote wawili watakatiliwa mbali na watu wao. 19#Law 18:12-14Usifunue utupu wa umbu la mama yako, wala umbu la baba yako; kwa kuwa huyo amefunua utupu wa jamaa yake ya karibu; watauchukua uovu wao. 20Tena mtu mume akilala na mke wa mjomba wake, ameufunua utupu wa mjomba wake; watauchukua uovu wao; watakufa bila kuzaa mwana. 21#Law 18:16Tena mtu mume akimtwaa mke wa nduguye, ni uchafu; ameufunua utupu wa nduguye; hao watakuwa hawana wana.
22 #
Law 18:26; 19:37 Basi zishikeni amri zangu zote, na hukumu zangu zote, na kuzifanya; ili kwamba hiyo nchi, ambayo nawapeleka ninyi kukaa, isiwatapike. 23#Kum 9:5Nanyi msiende kwa kuziandama desturi za taifa, niitoayo mbele yenu; kwa kuwa wao waliyafanya mambo hayo yote, na kwa ajili ya hayo niliwachukia. 24#Kut 3:17; 6:8; 19:5; 33:16; Kum 7:6; 14:2; 1 Fal 8:53; Zab 135:4; 1 Pet 2:9Lakini mimi nimewaambia ninyi, Mtairithi nchi yao, nami nitawapa ninyi kuimiliki; nchi iliyojaa maziwa na asali; mimi ni BWANA, Mungu wenu, niliyewatenga ninyi na mataifa. 25#Law 11:47; Kum 14:4Kwa ajili ya hayo mtapambanua kati ya mnyama aliye safi na mnyama aliye najisi, na kati ya ndege aliye tohara na ndege aliye najisi; nanyi msizifanye nafsi zenu kuwa machukizo kwa njia ya mnyama, au kwa njia ya ndege, au kwa njia ya kitu cho chote ambacho nchi imejaa nacho, niliowatenga nanyi kuwa ni najisi. 26#Law 19:2; Zab 99:5; Isa 6:3; 30:11; 1 Pet 1:16; Ufu 3:7; 4:8; Tit 2:14Nanyi mtakuwa watakatifu kwangu mimi; kwa kuwa mimi BWANA ni mtakatifu nami nimewatenga ninyi na mataifa, ili kwamba mwe wangu.
27 #
Kut 22:18; Kum 18:10; 1 Sam 28:7 Tena mtu mume au mtu mke aliye na pepo, au aliye mchawi, hakika atauawa; watawapiga kwa mawe; damu yao itakuwa juu yao.
Iliyochaguliwa sasa
Law 20: SUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.