Ayu 33
33
Elihu Amkemea Ayubu
1 #
Ayu 13:6
Walakini, Ayubu, nakuomba usikilize matamko yangu,
Ukayasikilize maneno yangu yote.
2Tazama basi, nimefunua kinywa changu,
Ulimi wangu umenena kinywani mwangu.
3 #
1 The 1:3
Maneno yangu yatatamka uelekevu wa moyo wangu;
Na hayo niyajuayo midomo yangu itayanena kwa unyofu.
4 #
Mwa 2:7
Roho ya Mungu imeniumba,
Na pumzi za Mwenyezi hunipa uhai.
5Kwamba waweza, nijibu;
Yapange maneno yako sawasawa mbele yangu, usimame.
6 #
Ayu 9:32
Tazama, mimi ni mbele ya Mungu kama ulivyo wewe;
Mimi nami nilifinyangwa katika udongo.
7 #
Ayu 13:21
Tazama, utisho wangu hautakutia hofu wewe,
Wala sitakulemea kwa uzito.
8Hakika umenena masikioni mwangu,
Nami nimesikia sauti ya maneno yako, ukisema,
9 #
Ayu 10:7
Mimi ni safi, sina makosa;
Sina hatia, wala hapana uovu ndani yangu;
10 #
Ayu 13:24
Tazama, yuaona sababu za kufarakana nami,
Hunihesabu kuwa ni adui yake;
11 #
Ayu 13:27
Hunitia miguu yangu katika mkatale,
Na mapito yangu yote huyapeleleza.
12 #
Mhu 7:20
Tazama, nitakujibu, katika neno hili huna haki;
Kwa maana Mungu ni mkuu kuliko mwanadamu.
13 #
Isa 45:9
Nawe kwani kumnung’unikia,
Kwa vile asivyotoa hesabu ya mambo yake yote?
14Kwa kuwa Mungu hunena mara moja,
Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali.
15 #
Ayu 4:13
Katika ndoto, katika maono ya usiku,
Usingizi mzito uwajiliapo watu,
Katika usingizi kitandani;
16Ndipo huyafunua masikio ya watu,
Na kuyatia muhuri mafundisho yao,
17Ili amwondoe mtu katika makusudio yake,
Na kumfichia mtu kiburi;
18Yeye huizuia nafsi yake isiende shimoni,
Na uhai wake usiangamie kwa upanga.
19 #
Kum 8:5; Zab 94:12,13 Yeye hutiwa adabu kwa maumivu kitandani mwake,
Na kwa mashindano yaendeleayo daima mifupani mwake;
20Hata roho yake huchukia chakula,
Na nafsi yake huchukia nyama nzuri.
21 #
Zab 102:5
Nyama ya mwili wake huliwa, isionekane;
Na mifupa yake isiyoonekana yatokea nje.
22Naam, nafsi yake inakaribia shimoni,
Na uhai wake unakaribia waangamizi.
23 #
2 Nya 36:15,16; Mal 2:7 Kwamba akiwapo malaika pamoja naye,
Mkalimani, mmoja katika elfu,
Ili kumwonyesha binadamu hayo yampasayo;
24 #
Rum 3:24
Ndipo amwoneapo rehema, na kusema,
Mwokoe asishuke shimoni;
Mimi nimeuona ukombozi.
25Nyama ya mwili wake itakuwa laini kuliko ya mtoto;
Huzirudia siku za ujana wake;
26 #
2 Fal 20:2-5; Zab 6:1-9 Yeye humwomba Mungu, naye akamtakabalia;
Hata auone uso wake kwa furaha;
Naye humrejezea mtu haki yake.
27Yeye huimba mbele ya watu, na kusema,
Mimi nimefanya dhambi, na kuyapotosha hayo yaliyoelekea,
Wala sikulipizwa jambo hilo;
28Yeye ameikomboa nafsi yangu isiende shimoni,
Na uhai wangu utautazama mwanga.
29Tazama, hayo yote ni Mungu anayeyafanya,
Mara mbili, naam, hata mara tatu, kwa mtu,
30 #
Zab 40:2; Zek 9:11 Ili kurudisha roho yake itoke shimoni,
Ili atiwe mwanga kwa mwanga wa walio hai.
31Angalia sana, Ee Ayubu, unisikilize;
Nyamaza, mimi nitasema.
32 #
2 Kor 1:24
Kama una neno la kusema, nijibu;
Nena, kwani nataka kukuhesabia kuwa na haki.
33 #
Zab 34:11
Kama sivyo, unisikilize mimi;
Nyamaza, nami nitakufunza hekima.
Iliyochaguliwa sasa
Ayu 33: SUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.