Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ayu 27

27
Ayubu Ashikilia Uelekevu Wake
1Kisha Ayubu akaendelea na mithali yake, na kusema,
2 # Ayu 34:5 Kama aishivyo Mungu, aliyeniondolea haki yangu;
Huyo Mwenyezi aliyeitesa nafsi yangu;
3(Kwa kuwa uhai wangu ukali mzima ndani yangu,
Na roho ya Mungu i katika pua yangu;)
4Hakika midomo yangu haitanena yasiyo haki,
Wala ulimi wangu hautatamka udanganyifu.
5 # Ayu 13:15 Hasha! Nisiwahesabie ninyi kuwa na haki;
Hata nitakapokufa sitajiondolea uelekevu wangu.
6 # Ayu 2:3; Mdo 24:16 Haki yangu naishika sana, wala sitaiacha;
Moyo wangu hautanisuta wakati nikiwapo hai.
7Adui yangu na awe kama huyo mwovu,
Na mwenye kuondoka kinyume changu na awe kama asiye haki.
8 # Mt 16:26 Kwani tumaini la mpotovu ni nini, ingawa ajipatia faida,
Hapo Mungu amwondoleapo roho yake?
9 # Mit 1:28; Isa 1:15; Mik 3:4; Zek 7:13; Yak 4:3 Je! Mungu atakisikia kilio chake,
Taabu zitakapomfikilia?
10 # Ayu 22:26 Je! Atajifurahisha katika Mwenyezi,
Na kumlingana Mungu nyakati zote?
11Nitawafundisha ninyi mambo ya mkono wa Mungu;
Hayo yaliyo kwa Mwenyezi sitayaficha.
12Tazama, ninyi nyote mmeyaona wenyewe;
Mbona basi mmebatilika kabisa?
13Hii ndiyo sehemu ya mtu mwovu kwa Mungu,
Na urithi wa hao waoneao, waupokeao kwa Mwenyezi.
14 # Kum 28:32,41; Est 9:10; 2 Fal 10:6-10 Watoto wake wakiongezeka ni kwa upanga;
Na wazao wake hawatashiba chakula.
15 # Zab 78:64 Hao watakaosalia kwake watazikwa katika kufa,
Wala wajane wake waliofiwa na waume hawataomboleza.
16Ajapokusanya fedha kama mavumbi,
Na kujifanyia mavazi kama udongo kwa wingi;
17 # Mit 28:8; Mhu 2:26 Yumkini kuyatengeza, lakini wenye haki watayavaa,
Nao wasio na hatia watazigawanya hizo fedha.
18 # Omb 2:6 Yeye hujenga nyumba yake kama mdudu,
Na kama kibanda afanyacho mlinzi.
19 # Hes 20:26 Yeye hujilaza hali ni tajiri, lakini ndio mwisho;
Hufunua macho yake, naye hayuko.
20Vitisho vyampata kama maji mengi;
Dhoruba humwiba usiku.
21Upepo wa mashariki humchukua, naye huondoka;
Na kumkumba atoke mahali pake.
22Kwani Mungu atamtupia asimhurumie;
Angependa kuukimbia mkono wake.
23Watu watampigia makofi,
Na kumzomea atoke mahali pake.

Iliyochaguliwa sasa

Ayu 27: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia