Ayu 26
26
Ayubu Ajibu: Ukuu wa Mungu Hauchunguziki
1Ndipo Ayubu akajibu, na kusema,
2 #
Mit 25:11
Jinsi ulivyomsaidia huyo asiye na uwezo!
Jinsi ulivyouokoa mkono usio na nguvu!
3 #
1 Kor 2:4
Jinsi ulivyomshauri huyo asiye na hekima!
Na kutangaza ujuzi wa kweli kwa wingi!
4Je! Umetamka maneno kwa nani?
Kisha ni roho ya nani iliyotoka kwako?
5Hao waliokufa watetema
Chini ya maji na hao wayakaao.
6 #
Zab 139:8; Mit 15:11; Isa 14:9; Amo 9:2; Ebr 4:13 Kaburi li wazi mbele yake,
Uharibifu nao hauna kifuniko.
7 #
Zab 24:1,2 Yeye hutandaza kaskazi juu ya nafasi isiyo na kitu,
Na kuutundika ulimwengu pasipo kitu.
8 #
Mit 30:4
Huyafunga maji ndani ya mawingu yake mazito;
Na hilo wingu halipasuki chini yake.
9Husitiri uso wa kiti chake cha enzi,
Na kulitandaza wingu lake juu yake.
10 #
Yer 5:22
Amepiga duara kuwa ni mpaka juu ya uso wa maji,
Hata hapo mwanga na giza vinapopakana.
11Nguzo za mbingu zatetemeka,
Na kustaajabu kwa kukemea kwake.
12 #
Kut 14:21; Isa 51:15; Zab 29:10; 74:13 Huichafua bahari kwa uwezo wake,
Na kumtema Rahabu kwa akili zake.
13 #
Zab 33:6
Hizo mbingu hupambwa kwa roho yake;
Mkono wake umemchoma nyoka aendaye mbio.
14Tazama, hivi ni viunga tu vya njia zake;
Na jinsi yalivyo madogo manong’ono tusikiayo katika habari zake!
Lakini ngurumo za uweza wake ni nani awezaye kuelewa nazo?
Iliyochaguliwa sasa
Ayu 26: SUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.