YouVersion Logo
Search Icon

Yn 7:1, 2, 3, 4, 5, 6, 8, 9, 10

Yn 7:1 SUV

Na baada ya hayo Yesu alikuwa akitembea katika Galilaya; maana hakutaka kutembea katika Uyahudi, kwa sababu Wayahudi walikuwa wakitafuta kumwua.

Yn 7:2 SUV

Na sikukuu ya Wayahudi, Sikukuu ya Vibanda, ilikuwa karibu.

Yn 7:3 SUV

Basi ndugu zake wakamwambia, Ondoka hapa, uende Uyahudi, wanafunzi wako nao wapate kuzitazama kazi zako unazozifanya.

Yn 7:4 SUV

Kwa maana hakuna mtu afanyaye neno kwa siri, naye mwenyewe ataka kujulikana. Ukifanya mambo haya, basi jidhihirishe kwa ulimwengu.

Yn 7:5 SUV

Maana hata nduguze hawakumwamini.

Yn 7:6 SUV

Basi Yesu akawaambia, Haujafika bado wakati wangu; ila wakati wenu sikuzote upo.

Yn 7:8 SUV

Kweeni ninyi kwenda kula sikukuu; mimi sikwei bado kwenda kula sikukuu hii, kwa kuwa haujatimia wakati wangu.

Yn 7:9 SUV

Naye alipokwisha kuwaambia hayo, alikaa vivi hivi huko Galilaya.

Yn 7:10 SUV

Hata ndugu zake walipokwisha kukwea kuiendea sikukuu, ndipo yeye naye alipokwea, si kwa wazi bali kana kwamba kwa siri.