YouVersion Logo
Search Icon

Yn 6:61, 62, 63, 64, 65, 66, 67, 68, 69, 70

Yn 6:61 SUV

Naye Yesu akafahamu nafsini mwake ya kuwa wanafunzi wake wanalinung’unikia neno hilo, akawaambia, Je! Neno hili linawakwaza?

Yn 6:62 SUV

Itakuwaje basi, mmwonapo Mwana wa Adamu akipaa huko alikokuwako kwanza?

Yn 6:63 SUV

Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima.

Yn 6:64 SUV

Lakini kuna wengine miongoni mwenu wasioamini. Kwa maana Yesu alijua tangu mwanzo ni nani wasioamini, naye ni nani atakayemsaliti.

Yn 6:65 SUV

Akasema, Kwa sababu hiyo nimewaambia ya kwamba hakuna mtu awezaye kuja kwangu isipokuwa amejaliwa na Baba yangu.

Yn 6:66 SUV

Kwa ajili ya hayo wengi miongoni mwa wanafunzi wake wakarejea nyuma, wasiandamane naye tena.

Yn 6:67 SUV

Basi Yesu akawaambia wale Thenashara, Je! Ninyi nanyi mwataka kuondoka?

Yn 6:68 SUV

Basi Simoni Petro akamjibu, Bwana! Twende kwa nani? Wewe unayo maneno ya uzima wa milele.

Yn 6:69 SUV

Nasi tumesadiki, tena tumejua, ya kuwa wewe ndiwe Mtakatifu wa Mungu.

Yn 6:70 SUV

Yesu akawajibu, Je! Mimi sikuwachagua ninyi Thenashara, na mmoja wenu ni shetani?

Video for Yn 6:61-70