YouVersion Logo
Search Icon

Yn 1:2, 3, 4, 5, 6, 7, 8, 9, 10, 11, 12, 13, 14, 15, 16, 17, 18

Yn 1:2 SUV

Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu.

Yn 1:3 SUV

Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.

Yn 1:4 SUV

Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu.

Yn 1:5 SUV

Nayo nuru yang’aa gizani, wala giza halikuiweza.

Yn 1:6 SUV

Palitokea mtu, ametumwa kutoka kwa Mungu, jina lake Yohana.

Yn 1:7 SUV

Huyo alikuja kwa ushuhuda, ili aishuhudie ile nuru, wote wapate kuamini kwa yeye.

Yn 1:8 SUV

Huyo hakuwa ile nuru, bali alikuja ili aishuhudie ile nuru.

Yn 1:9 SUV

Kulikuwako Nuru halisi, amtiaye nuru kila mtu, akija katika ulimwengu.

Yn 1:10 SUV

Alikuwako ulimwenguni, hata kwa yeye ulimwengu ulipata kuwako, wala ulimwengu haukumtambua.

Yn 1:11 SUV

Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea.

Yn 1:12 SUV

Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake

Yn 1:13 SUV

waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.

Yn 1:14 SUV

Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.

Yn 1:15 SUV

Yohana alimshuhudia, akapaza sauti yake akasema, Huyu ndiye niliyenena habari zake ya kwamba, Ajaye nyuma yangu amekuwa mbele yangu; kwa maana alikuwa kabla yangu.

Yn 1:16 SUV

Kwa kuwa katika utimilifu wake sisi sote tulipokea, na neema juu ya neema.

Yn 1:17 SUV

Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa; neema na kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo.

Yn 1:18 SUV

Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote; Mungu Mwana pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyemfunua.