Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yer 28

28
Hanania Ampinga Yeremia na Kufa
1 # Yer 27:1; 36:12; 2 Tim 2:8; 2 Pet 2:1; 2 Fal 24:18-20; 2 Nya 36:11-13 Ikawa, katika mwaka ule ule, mwanzo wa kutawala kwake Sedekia, mfalme wa Yuda, mwaka wa nne, mwezi wa tano, Hanania, mwana wa Azuri, nabii, wa Gibeoni, akasema nami ndani ya nyumba ya BWANA, mbele ya makuhani na watu wote, akisema, 2#Yer 27:12BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nimeivunja nira ya mfalme wa Babeli. 3#2 Fal 24:13; 2 Nya 36:10; Yer 27:16-22Kabla haujatimia muda wa miaka miwili mizima, nitavirudisha mahali hapa vyombo vyote vya nyumba ya BWANA, ambavyo Nebukadreza, mfalme wa Babeli, aliviondoa katika mahali hapa, akavichukua mpaka Babeli. 4Nami nitamrudisha hapa Yekonia, mwana wa Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, pamoja na mateka wote wa Yuda, waliokwenda Babeli, asema BWANA; maana nitaivunja nira ya mfalme wa Babeli. 5Ndipo nabii Yeremia akamwambia nabii Hanania, mbele ya makuhani, na mbele ya watu wote waliosimama ndani ya nyumba ya BWANA, 6#1 Fal 1:36; 1 Nya 16:36; Zab 41:13; 72:19; 89:52; Mit 6:13; 1 Kor 14:16; 2 Kor 1:20; Ufu 1:18naam, nabii Yeremia akasema, Amina, BWANA na atende hivi; BWANA ayatimize maneno yako uliyotabiri, kuvirudisha hapa vyombo vya nyumba ya BWANA na watu wote waliofungwa, toka Babeli, hata mahali hapa. 7Lakini lisikilize sasa neno hili nilisemalo, masikioni mwako, na masikioni mwa watu wote, 8Manabii waliokuwako kabla ya zamani zangu, na zamani zako, walitabiri juu ya nchi nyingi, na juu ya falme kubwa, habari ya vita, na ya mabaya, na ya tauni. 9#Kum 18:22; Isa 8:20Nabii atabiriye habari za amani, neno la nabii yule litakapotokea, ndipo nabii yule atakapojulikana, kuwa BWANA amemtuma kweli kweli. 10#1 Fal 22:24; Zab 10:13Ndipo nabii Hanania akaitwaa hiyo nira iliyokuwa juu ya shingo ya Yeremia, akaivunja. 11#Yer 27:7; Mit 26:4Naye Hanania akanena mbele ya watu wote, akisema, BWANA asema hivi, Hivyo ndivyo nitakavyoivunja nira ya Nebukadreza, mfalme wa Babeli, kabla haujatimia muda wa miaka miwili mizima, na kuiondoa shingoni mwa mataifa yote. Basi nabii Yeremia akaenda zake.
12Ndipo neno la BWANA likamjia Yeremia, baada ya Hanania, nabii, kuivunja ile nira iliyokuwa juu ya shingo ya Yeremia, kusema, 13Enenda ukamwambie Hanania, ukisema, BWANA asema hivi, Umezivunja nira za mti; lakini badala yake utafanya nira za chuma. 14#Kum 28:48; Yer 27:4-7Maana BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nimetia nira ya chuma juu ya shingo ya mataifa haya yote, ili wamtumikie Nebukadreza, mfalme wa Babeli nao watamtumikia; nami nimempa wanyama wa nchi pia. 15#Yer 20:6; 29:31Kisha nabii Yeremia akamwambia nabii Hanania, Sikia sasa, Ee Hanania; BWANA hakukutuma; lakini unawatumainisha watu hawa maneno ya uongo. 16Basi BWANA asema hivi, Tazama, nakutuma uende zako toka juu ya uso wa nchi; mwaka huu utakufa, kwa sababu umenena maneno ya uasi juu ya BWANA. 17#Kum 32:35; 1 Sam 2:9; Ayu 21:30; Mit 11:21; Zab 9:16; 34:21; Nah 1:2,3; Rum 2:2,3; Ebr 9:27; 12:29Basi nabii Hanania akafa, mwaka uo huo, mwezi wa saba.

Iliyochaguliwa sasa

Yer 28: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha