Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yak 5

5
Onyo kwa Matajiri Wadhalimu
1 # Lk 6:24 Haya basi, enyi matajiri! Lieni, mkapige yowe kwa sababu ya mashaka yenu yanayowajia. 2#Mt 6:19Mali zenu zimeoza, na mavazi yenu yameliwa na nondo. 3#Mit 16:27Dhahabu yenu na fedha yenu zimeingia kutu, na kutu yake itawashuhudia, nayo itakula miili yenu kama moto. Mmejiwekea akiba katika siku za mwisho. 4#Kum 24:14-15; Law 19:13; Mal 3:5; Isa 5:9; Ayu 31:38-40Angalieni, ujira wa wakulima waliovuna mashamba yenu, ninyi mliouzuia kwa hila, unapiga kelele, na vilio vyao waliovuna vimeingia masikioni mwa Bwana wa majeshi. 5#Lk 16:19,25; Yer 12:3Mmefanya anasa katika dunia, na kujifurahisha kwa tamaa; mmejilisha mioyo yenu kama siku ya machinjo. 6Mmehukumu mwenye haki mkamwua; wala hashindani nanyi.
Uvumilivu katika Mateso
7 # Kum 11:14; Yoe 2:23; Zek 10:1; Yer 5:24; Lk 21:19; Ebr 10:36 Kwa hiyo ndugu, vumilieni, hata kuja kwake Bwana. Tazama, mkulima hungoja mazao ya nchi yaliyo ya thamani, huvumilia kwa ajili yake hata yatakapopata mvua ya kwanza na ya mwisho. 8#Ebr 10:25; 1 The 2:16; 3:13Nanyi vumilieni, mthibitishe mioyo yenu, kwa maana kuja kwake Bwana kunakaribia.
9Ndugu, msinung’unikiane, msije mkahukumiwa. Angalieni, mwamuzi amesimama mbele ya milango. 10#Mt 5:12Ndugu, watwaeni manabii walionena kwa jina la Bwana, wawe mfano wa kustahimili mabaya, na wa uvumilivu. 11#Ayu 1:21-22; 2:10; Zab 103:8; 111:4; Dan 12:12Angalieni, twawaita heri wao waliosubiri. Mmesikia habari ya subira yake Ayubu, mmeuona mwisho wa Bwana ya kwamba Bwana ni mwingi wa rehema, mwenye huruma.
12 # Mt 5:34-37 Lakini zaidi ya yote, ndugu zangu, msiape, wala kwa mbingu wala kwa nchi; wala kwa kiapo kinginecho chote; bali ndiyo yenu na iwe ndiyo, na siyo yenu iwe siyo, msije mkaangukia hukumu.
Sala ya Imani
13 # Zab 50:15; Kol 3:16 Mtu wa kwenu amepatikana na mabaya? Na aombe. Ana moyo wa kuchangamka? Na aimbe zaburi. 14#Mk 6:13Mtu wa kwenu amekuwa hawezi? Na awaite wazee wa kanisa; nao wamwombee, na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana. 15#Mk 16:18Na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa yule, na Bwana atamwinua; hata ikiwa amefanya dhambi, atasamehewa. 16Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii. 17#1 Fal 17:1; 18:1; Lk 4:25; Mdo 14:15Eliya alikuwa mwanadamu mwenye tabia moja na sisi, akaomba kwa bidii mvua isinyeshe, na mvua haikunyesha juu ya nchi muda wa miaka mitatu na miezi sita. 18#1 Fal 18:42-45Akaomba tena, mbingu zikatoa mvua, nayo nchi ikazaa matunda yake.
19 # Gal 6:1 Ndugu zangu, ikiwa mtu wa kwenu amepotelea mbali na kweli, na mtu mwingine akamrejeza; 20#Mit 10:12; 1 Pet 4:8; Zab 51:13jueni ya kuwa yeye amrejezaye mwenye dhambi hata atoke katika njia ya upotevu, ataokoa roho na mauti, na kufunika wingi wa dhambi.

Iliyochaguliwa sasa

Yak 5: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia