Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Isa 47

47
Kuaibishwa kwa Babeli
1 # Yer 48:18; Omb 2:3,10; Isa 13:1—14:23; Yer 50:1—51:64 Haya, shuka, keti mavumbini,
Ewe bikira, binti Babeli;
Keti chini pasipo kiti cha enzi,
Ewe binti wa Wakaldayo;
Maana hutaitwa tena mwororo, mpenda anasa.
2 # Kut 11:5 Twaa mawe ya kusagia, usage unga;
Vua utaji wako, ondoa mavazi yako,
Funua mguu wako, pita katika mito ya maji.
3 # Nah 3:5; Mt 7:2; Rum 12:19 Uchi wako utafunuliwa,
Naam, aibu yako itaonekana.
Nitalipa kisasi; simkubali mtu ye yote.
4Mkombozi wetu, BWANA wa majeshi ndilo jina lake,
Mtakatifu wa Israeli.
5 # 1 Sam 2:9; Dan 2:37 Kaa kimya, ingia gizani,
Ee binti wa Wakaldayo;
Maana hutaitwa tena Malkia wa falme.
6 # 2 Nya 28:9; Isa 10:6; Zek 1:15; Kum 28:50 Nalikuwa nimekasirika na watu wangu, naliutia unajisi urithi wangu, nikawatia mkononi mwako; wewe hukuwatendea rehema; uliwatia wazee nira yako, nayo nzito sana. 7#Ufu 18:7Ukasema, Mimi nitakuwa bibi milele; hata hukuyatia hayo moyoni mwako, wala hukukumbuka mwisho wa mambo hayo.
8 # Sef 2:15; Ufu 18:7-8 Sasa, basi, sikia haya, wewe upendaye anasa, ukaaye na kujiona salama, wewe usemaye moyoni mwako, Mimi ndiye, wala hapana mwingine zaidi yangu mimi; sitaketi mfano wa mjane, wala sitajua kufiwa na watoto; 9#1 The 5:3; Dan 2:2; Nah 3:4; 2 The 2:9,10; Ufu 9:21lakini mambo haya mawili yatakupata katika dakika moja siku moja, kufiwa na watoto, na ujane; yatakupata kiasi kitimilifu, uchawi wako ujapokuwa mwingi, na uganga wako mwingi mno. 10#Zab 52:7; Eze 8:12Maana umeutumainia ubaya wako; umesema, Hapana anionaye; hekima yako, na maarifa yako yamekupotosha, nawe umesema moyoni mwako, Mimi ndiye, wala hapana mwingine zaidi yangu mimi. 11#Isa 13:6; Dan 5:30; Lk 17:27Kwa sababu hiyo ubaya utakupata; wala hutajua kutopoa kwake; na msiba utakuangukia; hutaweza kuuondoa; na ukiwa utakupata kwa ghafula, usioujua. 12Simama sasa na uganga wako, na wingi wa uchawi wako, uliojitaabisha nao tangu ujana wako; labda utaweza kupata faida, labda utaweza kushinda. 13Umechoka kwa wingi wa mashauri yako; basi, na wasimame hao wajuao falaki, wazitazamao nyota, watabirio kila mwezi mambo ya mwezi huo, wakakuokoe na mambo yatakayokupata. 14#Nah 1:10; Mal 4:1Tazama, watakuwa kama mabua makavu; moto utawateketeza; hawatajiokoa na nguvu za mwali wa moto; hautakuwa kaa la kukota moto, wala moto wa kukaa karibu nao. 15#Ufu 18:11Ndivyo yatakavyokuwa mambo hayo uliyojitaabisha nayo; wale waliofanya biashara nawe tangu ujana wako watatanga-tanga mbali nawe, kila mtu akienda zake; hapatakuwa na mtu wa kukuokoa.

Iliyochaguliwa sasa

Isa 47: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia