Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Isa 35

35
Kurudi Sayuni kwa Waliokombolewa
1Nyika na mahali palipo ukiwa patafurahi; jangwa litashangilia na kuchanua maua kama waridi. 2Litachanua maua mengi, na kufurahi, naam, kwa shangwe na kuimba; litapewa uzuri wa Lebanoni, utukufu wa Karmeli na Sharoni; watauona utukufu wa BWANA, ukuu wa Mungu wetu.
3 # Ayu 4:3,4; Ebr 12:12 Itieni nguvu mikono iliyo dhaifu, yafanyeni imara magoti yaliyolegea. 4Waambieni walio na moyo wa hofu, Jipeni moyo, msiogope; tazama, Mungu wenu atakuja na kisasi, na malipo ya Mungu; atakuja na kuwaokoa ninyi. 5#Isa 29:18; Yn 9:6; Mt 9:27; 11:5; Mk 7:32; Lk 7:22Ndipo macho ya vipofu yatafumbuliwa, na masikio ya viziwi yatazibuliwa. 6#Lk 7:22; Yn 5:8; Mdo 3:2; Mt 9:32; Yn 7:38Ndipo mtu aliye kilema ataruka-ruka kama kulungu, na ulimi wake aliye bubu utaimba; maana katika nyika maji yatabubujika; na vijito jangwani. 7Na mchanga ung’aao mfano wa maji utakuwa ziwa la maji, na nchi yenye kiu itakuwa chemchemi za maji; katika makao ya mbweha, walipokuwa wamelala, patakuwa na majani, pamoja na mianzi na manyasi. 8#Yoe 3:17; Ufu 21:27Na hapo patakuwa na njia kuu, na njia, nayo itaitwa, Njia ya utakatifu; wasio safi hawatapita juu yake; bali itakuwa kwa ajili ya watu hao; wasafirio, wajapokuwa wajinga, hawatapotea katika njia hiyo. 9#Law 26:6; Isa 11:9Hapo hapatakuwa na simba, wala mnyama mkali hatapanda juu yake; hawataonekana hapo; bali waliokombolewa watakwenda katika njia hiyo. 10#Isa 51:11; 25:8; Efe 1:7; Ufu 7:17; Yn 16:22Na hao waliokombolewa na BWANA watarudi, watafika Sayuni wakiimba; na furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao; nao watapata kicheko na furaha, huzuni na kuugua zitakimbia.

Iliyochaguliwa sasa

Isa 35: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha