Ebr 13
13
Huduma Impendezayo Mungu
1 #
Yn 13:34; 2 Pet 1:7 Upendano wa ndugu na udumu. 2#Mwa 18:1-8; 19:1-3; Rum 12:13; 1 Pet 4:9Msisahau kuwafadhili wageni; maana kwa njia hii wengine wamewakaribisha malaika pasipo kujua. 3#Mt 25:36Wakumbukeni hao waliofungwa kana kwamba mmefungwa pamoja nao; na hao wanaodhulumiwa, kwa vile ninyi nanyi mlivyo katika mwili. 4#Gal 5:19,21; Efe 5:5Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu. 5#Kum 31:6,8; Yos 1:5; 1 Tim 6:6Msiwe na tabia ya kupenda fedha; mwe radhi na vitu mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa. 6#Zab 118:6Hata twathubutu kusema,
Bwana ndiye anisaidiaye, sitaogopa;
Mwanadamu atanitenda nini?
7 #
1 Kor 4:16
Wakumbukeni wale waliokuwa wakiwaongoza, waliowaambia neno la Mungu; tena, kwa kuuchunguza sana mwisho wa mwenendo wao, iigeni imani yao. 8#1 Kor 3:11; Ufu 1:17Yesu Kristo ni yeye yule, jana na leo na hata milele. 9#Efe 4:14; Rum 14:17; 2 Kor 1:21Msichukuliwe na mafundisho ya namna nyingine nyingine, na ya kigeni; maana ni vizuri moyo ufanywe imara kwa neema, wala si kwa vyakula, ambavyo wao waliokwenda navyo hawakupata faida. 10#Ebr 8:4,5Tuna madhabahu ambayo wale waihudumiao ile hema hawana ruhusa kula vitu vyake. 11#Law 16:27Maana wanyama wale ambao damu yao huletwa ndani ya patakatifu na kuhani mkuu kwa ajili ya dhambi, viwiliwili vyao huteketezwa nje ya kambi. 12#Mt 21:39; Yn 9:22Kwa ajili hii Yesu naye, ili awatakase watu kwa damu yake mwenyewe, aliteswa nje ya lango. 13#Ebr 11:26; 12:2Basi na tutoke tumwendee nje ya kambi, tukichukua shutumu lake. 14#Ebr 11:10; 12:22Maana hapa hatuna mji udumuo, bali twautafuta ule ujao. 15#Law 7:12; 2 Nya 29:31; Zab 50:14,23; Isa 57:19; Hos 14:2Basi, kwa njia yake yeye, na tumpe Mungu dhabihu ya sifa daima, yaani, tunda la midomo iliungamayo jina lake. 16#Flp 4:18Lakini msisahau kutenda mema na kushirikiana; maana sadaka kama hizi ndizo zimpendezazo Mungu.
17 #
1 The 5:12; Eze 3:17 Watiini wenye kuwaongoza, na kuwanyenyekea; maana wao wanakesha kwa ajili ya roho zenu, kama watu watakaotoa hesabu, ili kwamba wafanye hivyo kwa furaha wala si kwa kuugua; maana isingewafaa ninyi.
18 #
2 Kor 1:12; Mdo 24:16 Tuombeeni; maana tunaamini kwamba tuna dhamiri njema, tukitaka kuwa na mwenendo mwema katika mambo yote. 19Nami nawasihi zaidi sana kufanya hayo ili nirudishwe kwenu upesi.
Baraka
20 #
Isa 63:11; 55:3; Zek 9:11; Yer 32:40; Eze 37:26; Yn 10:12; 1 Pet 2:25 Basi, Mungu wa amani aliyemleta tena kutoka kwa wafu Mchungaji Mkuu wa kondoo, kwa damu ya agano la milele, yeye Bwana wetu Yesu, 21awafanye ninyi kuwa wakamilifu katika kila tendo jema, mpate kuyafanya mapenzi yake, naye akifanya ndani yetu lipendezalo mbele zake, kwa Yesu Kristo; utukufu una yeye milele na milele. Amina.
Himizo za Mwisho na Salamu
22 #
Yak 1:21
Lakini nawasihi, ndugu, mchukuliane na neno hili lenye maonyo maana nimewaandikia kwa maneno machache. 23Jueni ya kuwa ndugu yetu Timotheo amekwisha kufunguliwa; ambaye, akija upesi, nitaonana nanyi pamoja naye.
24Wasalimuni wote wenye kuwaongoza, na watakatifu wote; hao walio wa Italia wanawasalimu.
25Neema na iwe nanyi nyote.
Iliyochaguliwa sasa
Ebr 13: SUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.